Hamisi Kigwangalah atoa shutuma dhidi ya Bashe

Huyu Kigwangallah inaonekana ana uhakika sana na hili suala la Uraia wa Hussein Bashe, kwa nini asimburuze kortini kabla ya uchaguzi ili amalize kazi mapema tu? Sema Magamba huwa manafiki tu haya...
 
Haya ni maneno ya mbunge wa Nzega Hamisi Kigwangalah aliyosema katika ukurasa wake wa facebook.

"Kuna mtu mmoja anahangaika jimboni
Nzega sasa hivi eti anazuia watu
wasilime pamba kwa kuwa Mbunge
amehamasisha kilimo hicho na watu
sasa wameitikia vizuri, na yeye
anaogopa wanavyozidi kuongezeka kwa kasi atashindwa kuniangusha
kirahisi 2015! Siasa za kipumbavu
namna hii hazitomsaidia, atamaliza hela
zake bure. Badala ya kuwasaidia
wazazi wake na ndugu zake anapita
akigawa pesa hovyo. Badala hata ya kujenga nyumba anapita akigawa pesa
na ahadi! Badala aanze kurekebisha
utata uliogubika uraia wake
anahangaika kuanza kampeni mapema
hii akipika pilau na nyama!"
mbona wote wana utata kuhusu uraia wao? Bashe raia wa Somalia na Kigwangala ni raia wa Burundi
 
Huyu Kigwangallah inaonekana ana uhakika sana na hili suala la Uraia wa Hussein Bashe, kwa nini asimburuze kortini kabla ya uchaguzi ili amalize kazi mapema tu? Sema Magamba huwa manafiki tu haya...

atathubutuuuuu...! Kigwangala mwenyewe ni Mrundi so ngoma droo wataendelea kusemana tu
 
hawa vijana mmoja yupo kwenye kundi la mzee wa viwango na speed mwingine yupo kwa mzee wa richmond. mwisho wao utategemea makundi yao
 
Back
Top Bottom