Hamis Tabasamu: Darasa la Saba aliyewashinda wasomi wabobezi kura za maoni CCM jimbo la Sengerema

Hii ina maanisha wasomi wetu elimu yao na vyeti vyao havina msaada kwa maisha ya mwananchi wa kawaida.
Hawa walitakiwa wakagombee kufundusha vyuoni.
Halafu jiulize mtu ni mhandisi, daktari anataka ubunge udaktari wake aluosomea anamuachia nani?
 
Wajumbe siyo watu ila most of them ni la saba
 
Mleta hoja kashabikia ujinga. Kwake Tanzania haina nafasi tena. Japo Sina utafiti, matokeo hayo yanaonesha ama matumizi makubwa ya pesa kununua wapiga kura, na/au kiwango kidogo cha elimu kwa wajumbe.
Sidhani. Wamewatendea haki acha wakafanye majukumu ya professional zao, wale wa Kilimo na Mifugo waende. Kuwakilisha wakulima haiitaji daktari wa meno
 
Tunangoja Waje Na Hayo Majina Dodoma
Watoa Rushwa Hawana Nafasi Wakatafute Kazi
Sawa. Kama Dodoma inapiga kura wakati wa uchaguzi leteni huyo wa Dodoma sanduku litaamua.
Ka.ma hitaji lilikuwa la wasomi ungewekwa mtihani sijui wa Law, uhasibu au udaktari
 
Kuna kamati mbalimbali, inawezekana kamati moja ikatumwa Kenya kwa jamboo maalumu mf. Mambo ya pesa na uchumi
 
Sawa!! Akienda bungeni ataweza kujenga hoja zilizoshiba? Kuna kamati mbalimbali bungeni, atawekwa wapi? Kwenye maswala ya kukutana na nchi jirani, atawaambia nini wasomi?
Tulipo fikia, kinacho hitajika ni uwezo wa kusifu tuuu
 
Inaonekana cdm Kuna vichwa Sana hata ukiwa std 7 ni sawa na degree holder tu,yaan std 7 ya CDM ni sawa na bachelor ya ccm
 
Kwa kifupi, wasomi wa Tz tumewaangusha Sana watz kwa miaka mingi iliyopita! Tuanze jitafakali Kama elimu zetu zimekuwa na Tija yoyote kwa wananchi wetu ambao hawakupata nafasi ya kubakia darasani!
 
Aisee hii kiboko,sidhani jama hao wasomi wana hamu na watu wa sengerema
 
kitu kimoja tukumbuke pia,hamisi amekuwa hapo sengerema miaka yote shughuli zake nyingi ni hapohao 24x7
hivyo maingiliano yake na wanasengerema hayawezi kuwa sawa na wasomi uliowataja kwa sbb wao wanaokana jimboni wakati kama huu tu
wa kupiga siasa, hamis for almost 15yrs 24x7amepiga siasa sengerema. fikiria tu mfanyabiashara mkubwa kautaka ubunge mara 3mfululizo ni wa hanuhanu anahudhuria vikao vya nzengo,harusi,misiba na michango anatoa. unategemea atakosa kura nyingi kwenye jamii zetu hizi eti sababu ya usomi?!!!?.Nampongeza kwa sababu hakukata tamaa amepigana sana hatimaye nuru kaanza kuiona naamini ana jambo kubwa anataka kuwafanyia wanasengerema tumuombee azidi kungára kwenye vikao vya juu.
KWA HIYO ISSUE HAPA SI USOMI.
 
Wapigakura wenyewe hawajielewi!

Wengi wao hawajui kama wabeba dhamana ya kuwakilisha wengi na hatima ya kiutendaji katika maisha yao
 
Mleta mada ni mjinga sana yapaswa aelimishwe sasa.
Kweli kabisa,mleta mada anatumika.Bila shaka kapewa rushwa pia.Huyo jamaa ni bepari,pamoja na kuwa na huo ukwasi bado ana njaa na tamaa ya kutaka kuingia bungeni.Anataka akafanye nini huko?kichaka cha kulinda mali zake.Kama ana pesa si alipe kodi tu na kuchangia shughuli za maendeleo.Bunge lijalo linahitaji brain za kukabiliana na wakenya na vita ya uchumi.Darasa la saba muda wao umeisha
 
Sawa!! Akienda bungeni ataweza kujenga hoja zilizoshiba? Kuna kamati mbalimbali bungeni, atawekwa wapi? Kwenye maswala ya kukutana na nchi jirani, atawaambia nini wasomi?
Kwani yule wa Makambako amewekwa kamati gani? Kama Tabasamu atapitishwa na baadaye kushinda, hatakuwa mbunge wa kwanza darasa la saba kutoka CCM. Kuna yule tajiri wa Makambako ambaye alicheza mayenu akikata kiuno baada ya kupitishwa katiba ya hovyo kwenye Bunge la Katiba. CCM wanaivuruga sana hii nchi, wanatengeneza mechanism ya kupeleka bungeni watu mbumbumbu wanaoweza kushangilia kila upuuzi utakaoletwa bungeni. Ukifanya utafiti, utagundua kuwa idadi kubwa ya wabunge mbumbumbu wanatoka CCM!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…