Hamis Tabasamu: Darasa la Saba aliyewashinda wasomi wabobezi kura za maoni CCM jimbo la Sengerema

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,234
Mfanyabiashara wa mafuta maarufu Hamis Tabasamu hivi karibuni ameshika nafasi ya kwanza kura za maoni CCM jimbo la Sengerema. Hamis Tabasamu mwenye elimu ya darasa la saba tu ameweza kuwashinda wasomi wabobezi wa maswala mbalimbali waliotia nia katika jimbo hilo

Mbali ya usomi wao lakini zaidi ni kumshinda Waziri mstaafu wa siku nyingi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo William Ngeleja

Hamis Tabasamu mwaka 2015 aligombea ubunge wa Sengerema kwa tiketi ya CHADEMA na kushindwa kumg'oa Ngeleja. Mwaka 2017 Tabasamu alihama CHADEMA na kwenda kuunga juhudi za Mheshimiwa John Magufuli kwa kile alichoita amechoshwa na upinzani kupinga kila kitu hasa hatua zilizochukuliwa kwenye makinikia

Wafuatao ndiyo walikuwa watia nia wa Sengerema

1. Hamis Tabasamu- Std 7
2. William Ngereja - Master in Law
3. Philemon Tano - Master in HRM
4. Joshua Shimiyu- Master in HRM
5. Lawrence Masha- Master in Law
6. Yohana Kasenga- Shahada ya elimu.
7. Ndakama Salang’anya- BA Econom
8. Kelvin Natto- BA in Law
9. Tumaini Limbe-Shahada ya Kilimo
na Mifugo
10. Yunge Maige- Bachelor ya Accounts
11. Mlyambelele Levi Ng'weli- Sheria + Post Graduate Diploma in Legal Practice.
12. Veronica K. Mugoyela- shahada ya Uzamivu fani ya Pharmacy.
13.William J.Tega PGD -Economic Diplomacy
14. Eng. Suleman Daudi Arthur Nkalango - Ph.D In Information and Telecommunication Engineering
15. Evarist Clement Matulanya- Shahada ya Ualimu
16.Dotto Joseph Ndemella-Master of Arts in Economics
17.Dr Godwin Silas Macheku,Adv.dipl (SRHR),MD(doctor of medicine),MMED (masters of medicine)(obgyn)
18. Onesmo Yegella Ntoneji, Masters in Procurement and supply chain management. PGD in Air Transport Management, (Airport operations)

Jimbo la Sengerema hawa ndio waliotia nia na namba 1 Ndo kashinda.
 
Kuna haja wagombea ambao ni wasomi kabla ya kwenda majimboni wakae chini na kujitafakari kwa kina sababu za kuelekea kushika nambari one ama kupata aibu kubwa. Vinginevyo wasomi wawe tayari kwenda kujifunza kwa std 7 namna ya kushinda kura haswa jinsi ya kupata kura za wajumbe wa kijijini
 
Kuna haja wagombea ambao ni wasomi kabla ya kwenda majimboni wakae chini na kujitafakari kwa kina sababu za kuelekea kushika nambari one ama kupata aibu kubwa. Vinginevyo wasomi wawe tayari kwenda kujifunza kwa std 7 namna ya kushinda kura haswa jinsi ya kupata kura za wajumbe wa kijijini
Kwa hali hii ni kweli unachokisema
 
Inawezekana upungufu wa elimu katika majimbo husika au Ni,Kama huyo jamaa Ni mfanyabiashara mkubwa Kama ulivyosema Basi alihonga Sana,wasomi hawajui kuhonga Kama wafanyabiashara.

Lakini kazi ya mbunge Ni kuwasiliana matatizo ya Wananchi bungeni ili yapangiwe bajeti ya utatuzi,suala la elimu hapo halipo,Kuna wasomi wengi ambao no Vilaza tu mfano Mwakyembe.Lakini Kuna wengine Ni darasa la Saba lakini huwezi kutofautisha na PhDs
 
KAMA HUJAFANYA UTAFITI AU HUNA INFORMATION UNAWEZA KUUAMINI HUU UZI.LAKINI UKWELI NI KWAMBA JAMAA KATOA RUSHWA YA KUFA MTU YEYE PAMOJA NA WAGOMBEA WENGINE ILI WAPATE KURA.WAGOMBEA WALIOKUWA WATIIFU KWA CHAMA KWA MAANA YA KUTOJIPITISHA NDIO WALIOPATA KURA MOJA AU SIFURI.RUSHWA ILIKUWA KUBWA MNO HAPO SENGEREMA NDIO MAANA SASA HIVI WANAFANYA PROPAGANDA KWENYE MITANDAO ILI KU NEUTRALIZE MADHAMBI YAO.WANATENGENEZA PROPAGANDA NA APPEAL FOR PITTY ILI DARASA LA SABA AHURUMIWE NA KUACHIWA USHINDI
 
KAMA HUJAFANYA UTAFITI AU HUNA INFORMATION UNAWEZA KUUAMINI HUU UZI.LAKINI UKWELI NI KWAMBA JAMAA KATOA RUSHWA YA KUFA MTU YEYE PAMOJA NA WAGOMBEA WENGINE ILI WAPATE KURA.WAGOMBEA WALIOKUWA WATIIFU KWA CHAMA KWA MAANA YA KUTOJIPITISHA NDIO WALIOPATA KURA MOJA AU SIFURI.RUSHWA ILIKUWA KUBWA MNO HAPO SENGEREMA NDIO MAANA SASA HIVI WANAFANYA PROPAGANDA KWENYE MITANDAO ILI KU NEUTRALIZE MADHAMBI YAO.WANATENGENEZA PROPAGANDA NA APPEAL FOR PITTY ILI DARASA LA SABA AHURUMIWE NA KUACHIWA USHINDI
Ngeleja kafanya nini la maana mpaka wajumbe wamchague tena ?Tabasamu yupo na wana Sengerema. Nyie kina Ngeleja,Masha n.k mnaishi Dar mnakuja tu kutafuta ubunge Sengerema. Mkafie mbele.
 
Uwezo wako mdogo sana,inawezekana hata darasa la saba hukumaliza.Ngeleja kaingiaje sasa kwenye post yangu?Sina muda wa kubishana na mtu mwenye ubongo mdogo na asiye na hoja
 
Sawa!! Akienda bungeni ataweza kujenga hoja zilizoshiba? Kuna kamati mbalimbali bungeni, atawekwa wapi? Kwenye maswala ya kukutana na nchi jirani, atawaambia nini wasomi?
Mleta hoja kashabikia ujinga. Kwake Tanzania haina nafasi tena. Japo Sina utafiti, matokeo hayo yanaonesha ama matumizi makubwa ya pesa kununua wapiga kura, na/au kiwango kidogo cha elimu kwa wajumbe.
 
Wasomi wa nchi hii ni shida Sana. Siyo Sengerema tu ambako wasomi wameangushwa, ni majimbo mengi.

Sababu kubwa ya wasomi kuamguka ni kukosa kitu kinaitwa "social chemistry" (yaani hawana muunganiko mzuri wa kijamii) na watu wa Jimbo husika.

Wasomi wanadhani watachaguliwa kwa kutaja madigrii yao na kuonesha magari yao ya mikopo kwa wajumbe. Bado wana fikra za mwaka 47 kwamba watu wanababaishwa na vitu wakasahau utu.

Ndiyo maana wengi wameangukia pua.
 
Wangechagua huyo Engineer au huyo MD kwa ustawi mzuri maana hao wana uwezekano mkubwa kuwa kwenye cabinet ijayo ukizingatia tena ni kanda pendwa na Mh ana ugonjwa na hizo Dr na Eng.

Majimbo ambayo hayajawahi kabisa kutoa waziri yeyote yanaongoza kwa kuwa nyuma kimaendeleo hasa yanapokuwa vijijini.
 
Darasa la saba si hoja, hoja ni ushindi kama kanuni au taratibu za uchaguzi.Na hilo ndio jambo muhimu.
Mbona mihemuko ya elimu iko huku kwetu mwisho wa dunia?Mbona ulaya ambako watu wamepata Phd miaka 200 na zaidi nyuma hawashangai kuona mbunge au kiongozi mwenye elimu ya chini?
What matters is the convincing power,ndio siri ya ushindi.Haya sio mashindano ya elimu.
 
Back
Top Bottom