kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 11,187
- 24,580
Hamas: Kutunguliwa ndege za Israel Gaza, ni ishara ya kuwa macho muqawama
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesema kitendo cha harakati hiyo kufanikiwa kutungua ndege za kijeshi za utawala wa Kizayuni wa Israel aina ya F-16 zinazoshambulia Ukanda wa Gaza ni ithibati tosha kuwa harakati hiyo ya muqawama imesimama kidete na iko tayari kuzima chokochoko na uvamizi wa Tel Aviv.
Katika taarifa iliyotolewa leo Alkhamisi, msemaji wa Hamas, Fawzi Barhoum sanjari na kupongeza ushujaa wa wanamapambano wa Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Hamas wakiongozwa na Mohammed Hajeila, waliouawa shahidi wakiwa katika jitihada za kutungua ndege hizo za Israel zilizokuwa zikilenga ngome za Hamas katika eneo la Shuja'iyyah mashariki mwa Ukanda wa Gaza, amesisitiza kuwa hujuma hizo za anga za ndege za Wazayuni hazitakuwa na matokeo mengine ghairi ya kuchochea ari na hamasa ya wanamuqawama hao.
Msemaji huyo wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amesema harakati hiyo inaunga mkono kundi lolote linalosimama dhidi ya utawala haramu wa Israel, na kwamba itatumia silaha zake wakati mwafaka kwa ajili ya kulenga maeneo lengwa na maadui.
Wapalestina kadhaa wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari wa utawala haramu wa Israel tangu yalipoanza maandamano ya Siku ya Ardhi yaliyopewa jina la "Haki ya Kurejea" yaliyoanza Ijumaa ya Machi 30 katika Ukanda wa Gaza.
Licha ya mauaji hayo, Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas amesisitiza kuwa maandamano makubwa ya amani yataendelea hadi pale mzingiro wa kibaguzi katika ukanda huo utakapoondolewa.