Hamadi Rashid na Cheyo kama CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamadi Rashid na Cheyo kama CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Watanzania, Feb 9, 2011.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimewasikiliza hawa wabunge jana wakiongea kama wabunge wa CCM. Hamadi Rashid anasema eti Spika ametupatia ushauri mzuri wabunge wa upinzani. Cheyo naye anasema eti siasa za nchi isitawalike. Sasa Hamadi Rashid na Cheyo wanasubiri nini kutangaza kuwa wao ni CCM damu damu?
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Hamadi Rashid ni sawa na Seif na Lipumba, kwao hawawezi kuishi bila madaraka ama kutambuliwa, Hamad anadhani CDM ndio wapinzani wao wakubwa, Ndio maana inashangaza movie ya ccm kung'ang'ania cuf , kwakua wanajua udhaifu wao, wanajua unyonge wao, wanajua cuf wanachotaka ni madaraka , ukiwapa wananyamaza kimya, wameona kule Znz, wametulizana kwa unyonge, ni waroho na warafi wa madaraka , ni genge la watu wahovyo, ooh Yes watu wa hovyo kabisa.
   
 3. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hawa jamaa walishafunga ndoa na CCM zamani sana!!!
   
 4. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Vipi ulimsikia Mbowe alivyo mbaguzi. Kwanini awabague wapinzani wenzake?
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Ni yaleyale tu ya divide the so that it becomes easier for you to rule them
   
 6. P

  Paul S.S Verified User

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kwa kipimo cha ufahamu wako upinzani maana yake ni kupinga kila kitu?
   
 7. A

  Anold JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Nafikiri matatizo yanayompata hamad pamoja na wenzake sasa hivi baada ya muafaka wa CCM na CUF ni jinsi gani wataweza kupenya nao kwenye serikali baada ya kiongozi wao seif kuwaacha solemba bila kuacha hatma yao. Kwa kweli wapo kwenye hali ngumu sana maana sasa hivi haieleweki kabisa nafasi ya wanachama wengine wa CUF kwenya huo muafaka kitu kinachofanya waishi na wafanye mambo kama watoto yatima. Hawa wameachwa solemba, sasa wasipojitahidi kupigana kupata sehemu ya kusimama hali itakuwa ngumu sana kwao. Siasa na wanasiasa wa tanzania sasa hivi ni kichekesho tosha maana ni maslahi kwanza kuwatumikia wananchi baadaye. Juzi nilitegemea makamu 2 wa rais wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar naye atakuwa miongoni mwa waandamanaji wa CUF wanaopinga malipo ya downs, lakini thubutu!! labda ni katika ukweli wa yule mtunga mashairi aliyewahi kuandika shairi lisemalo "kwetu ni kwenu kwa nini?" ngoja niishie hapa niangalie hii video ya vichekesho vya tz
   
 8. M

  Mwera JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  waroho na walafi Wa madaraka ni chama chenu cha kikabila chadema,bila ubinafsi na uroho wao wamadaraka yote haya yasingekuepo,sasa wameula wa chuya kwa tamaa zakijinga,
   
 9. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,881
  Trophy Points: 280
  Hivi wengine mpaka mpigwe nyundo ya kichwa ndio muelewe? sababu za CDM kuikataa CUF mbona zilishawekwa wazi mara nyingi.
  Hivi unaweza kumlazimisha mwanao kuoa wakati kesha kuambia "mzazi wangu, simtaki huyu ni malaya" ?
   
 10. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  Anayetoa hoja kanuni zibadilishwe ili apate madaraka na anayesimamia kanuni kama zinavyotaka ni yupi aliye mlafi wa madaraka?
   
 11. i

  ibange JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  unamaanisha chadema ni chama cha kabila gani? wapo kuanzia mtwara hadi kagera. labda ni cha kabila linaitwa tanganyika
   
Loading...