Hamad wa CUF atetea shavu lake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamad wa CUF atetea shavu lake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ugaibuni, Jan 10, 2012.

 1. u

  ugaibuni Member

  #1
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbunge wa Wawi kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF ambaye katika siku za karibu alifukuzwa uanachama na baadae mahakama kuzuia hatua fuatilizi mpaka kesi hiyo itakapokamilishwa leo ameenda mahakamani kuwasilisha hati juu ya kukiukwa kwa maamuzi ya mahakama yanayofanywa na Chama hicho.  Katika mahojiano ambayo tumeyaambatanisha hapo juu, kama ukisikilza na kutafakari kwa undani maneno na ari ya mbunge huyu utagundua kuwa anatumia nguvu kutetea shavu lake. Sasa kama ndani ya chama kimoja watu hamuelewani kuna maendeleo hapo? Siongei mengi zaidi ya kuwasilisha na kutaka mchango wenu wana Ughaibuni.com. Oooh! nilisahau kumbe bungeni kuna posho nono na nyingine inaongezwa punde. Naomba uangalie video hii halafu utoe maoni nini kina kuja akilini mwako, nini kama mwana Ughaibuni unamshauri huyu Mbunge?

  Chanzo: Ughaibuni.com
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. z

  zamlock JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  sasa si anajua bila bungeni atafanya nn tena biashara awezi si atakosa hata pesa ya mafuta kwenye gari
   
 3. T

  Topical JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Truce be told; hamad rashid hakustahili kufukuzwa uanachama, wangeweza ku-handle hiyo issue kwa busara zaidi na kusikiliza maoni yake, Maalim seif anazidii kuwa mfalme badala ya kiongozi
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Jan 10, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hakustahili kufukuzwa lakini ndio kisha fukuzwa..Mahakama sidhani kaa inaweza kuingilia maswala ya uanachama unless kuna sheria zaidi ya kanuni za chama. Kama HR hakuvunja kanuni za chama chake kama mwanachama, pengine ana nafasi lakini kama kweli kavunja kanuni ya chama who fires him haihusu mahakama..

  JK anaweza kumwachisha madaraka waziri, vunja bunge au kubadilisha baraza la mawaziri na mahakama isihusishwe!..Na sidhani kama tunahitaji kuweka sheria ambayo mbunge hawezi kufukuzwa na chama bali tunaweza boresha kanuni na misingi ya uanachama ktk vyama vya siasa ambazo zitatumika kwa vyama vyote kisheria..
  Nje ya hapo akubali matokeo, akagombea upya chini ya Jahazi Asilia au chama kinginecho.. Si kasema ataunda chama chake, tishio kama hili pekee inamweka pabaya zaidi..
   
 5. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Naikumbuka hoja ya Mwanakijiji "lazima kuheshimu ukuu wa chama ukishajiunga'.
   
 6. T

  Taso JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Ninavyoijua Tanzania yangu, inawezekana kabisa amri ilitolewa na mahakama halafu ikabaki inazagaa zagaa kwenye ma deski kati ya makarani na mahakimu na haikufika mkononi wa CUF timely.

  Ushaenda mahakamani ukaona hakimu ana scribble amri kwenye ki scratch paper halafu anakupa wewe litigant uende mtaani umchapishie umrudishie karani, karani ampe atie sahihi halafu anakurudishia wewe tena ndio uipeleke kunako husika, mshaona hizo? Itafika hiyo court order?
   
Loading...