Hamad rRashid aiteka Wawi

Amewasili na Kundi la waandishi kutoka tzbara.
Meli 5 ziliwasili zikitokea Tanzania bara kupitia Unguja.
Hoteli za Chake Chake zimejaa wageni waliopanga kuhudhuria mkutano huo.
Jana watu wa mikoa tofauti ya TZ bara walikuwa wakitembea tembea madukani kufanya Shopping ya viitu vya majumbani(electronic)
ndege 3 zikitokea dar zitawasili saa 4:30 kuelekea uwanjani moja kwa moja
amelipia mabilion ya shilingi kwa Redio ya Zenj Ifm ili kurusha matangazo yake moja kwa moja kutokea uwanja wa mapambano

Hii habari imekaa kwa kutengenezwa,mwandikaji amewezaje kufuatilia mambo hayo yote!!?hata kama ni kweli hizo pesa zimetoka wapi??kauli ile kuwa huyu jamaa anatumwa na watu sasa inaanza kuniingia kichwani,mtu unaweza kujimaliza huku ukifikiri kuwa unajiimalisha,hata hivyo kila la kheri.
 
Kama hii ni habari ya kweli basi ni kweli HR ametumwa na CCM(huyu na pinda ni marafiki na nadhani pia wote ni UWT) kuugawa upinzani. Ametoa wapi fedha za kufuru namna hiyo? Nadhani chadema wakae mkao wa mapambano maana anaweza kuja chadema au kuanzisha chama mbadala ambacho kitakuwa financed na ccm kwaajili ya kuwagawa wapinzani. Nadhani amemaliza kazi yake kule CUF sasa anapewa tena kazi nyingine.

Ataweza kupambana na watu makini kama chadema?
 
Mwakilishi wetu wa jussa kashawamaliza watanganyika, wamebaki kumtumia hamad rashid kutapatapa
 
sasa kama yy ana mass pemba - hizo meli tano alizochukua kutoka dar ni zanini???

hii habari sioni kama ina ukweli
 
Amewasili na Kundi la waandishi kutoka tzbara.
Meli 5 ziliwasili zikitokea Tanzania bara kupitia Unguja.
Hoteli za Chake Chake zimejaa wageni waliopanga kuhudhuria mkutano huo.
Jana watu wa mikoa tofauti ya TZ bara walikuwa wakitembea tembea madukani kufanya Shopping ya viitu vya majumbani(electronic)
ndege 3 zikitokea dar zitawasili saa 4:30 kuelekea uwanjani moja kwa moja
amelipia mabilion ya shilingi kwa Redio ya Zenj Ifm ili kurusha matangazo yake moja kwa moja kutokea uwanja wa mapambano
Picha mkuu..,tuwekee picha......:behindsofa:..!
 
Hamad rashid amewasili na meli kutokea znz. kabla ya hapo alikmutana na mkurugenzi wa Zenj IFM pale Momabasa ili kuweka mkakati wa kurusha matangazo yake. 1.5 billion zimemtoka ili kuitangaza ziara yake
 
Amewasili na Kundi la waandishi kutoka tzbara.
Meli 5 ziliwasili zikitokea Tanzania bara kupitia Unguja.
Hoteli za Chake Chake zimejaa wageni waliopanga kuhudhuria mkutano huo.
Jana watu wa mikoa tofauti ya TZ bara walikuwa wakitembea tembea madukani kufanya Shopping ya viitu vya majumbani(electronic)
ndege 3 zikitokea dar zitawasili saa 4:30 kuelekea uwanjani moja kwa moja
amelipia mabilion ya shilingi kwa Redio ya Zenj Ifm ili kurusha matangazo yake moja kwa moja kutokea uwanja wa mapambano

did you mean 'billions' of shillings?
Au macho yangu yana tatizo?
 
Nikiwa kama Mpemba naandika kwa herufi kubwa; "HAMADI RASHIDI ANAJIMALIZA", au atakua anatumiliwa na lakini vyovyote itakavyokua huu ni mwisho wake! Hebu fikiria, katoa gari pemba mzima ziende kwenye mkutano wake tena kila kijiji zimetoka gari kuanzia 4 na kwenda mbele na watu (wanaofata ngoma, wanawake, uroda wa gari, matembezi, kofia, fulana, vijisenti vya sabuni, mlo nk) wamepanda bure, kalipia studio itangaze mkutano, kakodi waandishi wa habari na watu mbali mbali kutoka Tanganyika. Hali hii CCM hawajawahi kuifanya! Wale wanaosema HR anataka kuimaliza CUF wajue anajimaliza mwenyewe na leo ndio anakuja kugongomelea msumari wa mwisho katika lenenza lake
 
Napeleka hongera zangu za moyo kabisa kwa Hamad Rashid kwa Ujasiri wake ,kujitowa kwenye shemere
za Seif na Jussa .Hamadi sema kweli bila ya kuitowa makali.Wakati umefika unafiki na uyakhe yakhe ukome.

Umiliki binafsi wa chama ukomeshwe - unafiki na masikilzano ya kisiri siri baina Jussa/Seif na AMANI
si halali katika Demokrasia ya leo .Ingawaje pamepatikana amani Visiwani kwa sababu ya MARIDHIANO ,lakini
usiri wa MARIDHIANO HAYO -ni dosari ambalo lazima kutia wasi wasi wananchi wote wa Visiwani na Wabara.
Makubaliano ya siri na chini kwa chini nio yanayofanya watu kuwalaumu Nyerere na Karume kuhusu Muungano.
Basi kwa nini waliypkubaliana baina ya Seif/Jussa na Amani hayawekwi hadharani ?

Hamadi Rashid ,alichohwa na mambo ya kisiri siri baina ya Jussa na Seif na hasa siasa ya uchochezi chochezi
na fitina a Jussa ,ndani ya chama cha CUF na kuhusu mahusiano baina ya Wavisiwani na Wabara .

Hekima ya HAMADI kuanzisha chama chake ni pigo kubwa la ile hutuma,uwongo na porojo la wapinzani wake
kuwa eti anatumiliwa na CCM au Chadema .

HAMADI Rashid ,TUMIA UHURU WAKO WA KUFIKIRI,KUJITAMKA NA KUCHAGUWA BILA WOGA NA HOFU.UHURU WAKO TUMIA.
Wanoogopa kutumia au unapotumika uhuru kama huo bila ya masharti hao maadui na niwapinzani wa Demokrasia.

UNDA CHAMA CHAKO NA WAPO WENGI TUTAKAO KUUNGA MKONO. SIASA ZA ZANZIBAR HAZINA MONOPOLY YA UBINAFSI AU
YA VYAMA MAKHSUS TU- UKWELI DAIMA UEMWE IJAPOKUA UNAUMA.
HAPANA UTUME KISIASA WALA WA UIONGOZI WA SIASA ,SI ZANZIBAR WALA TANZANIA BARA - TANGANYIKA .
Uishi Ujasiri wa HAMAD RASHID !!!
DEMOKRASIA OYEE!!
 
mambo ya kipemba hayo mi nawaachia wenyewe. Wakimaliza kubaguana hawatakuwa na nhuvu ya kutubagua

kwani hata bara ubaguzi si umejaa, kwani msukuma hana nafasi ktk jamii. Mchaga nae ni mbaguz mkubwa hata maji hatoi kwa mmasai
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom