G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 12,288
- 38,908
Kura mbili za rasimu zimepatikana kutoka kwa Hamad Rashidi mbunge wa Wawi imefahamika mjini Dodoma leo.
Katika hali ya kushangaza, Hamad Rashidi ndiye aliyepewa jukumu la kuwanunua wabunge wawili wa CUF (majina yanahifadhiwa) ili kukidhi akidi iliyotakiwa.
Wabunge hao ambao walikuwa wajumbe wa bunge maalum la katiba kabla ya kususia waliahidiwa kiasi cha shilingi milioni 250 za Kitanzania kila mmoja ili kufanikisha mpango huo. Aidha Hamad ndiye aliyepewa jukumu hilo la kuwashawishi huku wale waliopiga kura za siri za 'HAPANA' wakiwekwa kitako na Pinda pamoja na Seif Idd ili kukamilisha mpango huo.
Hamad Rashidi kwa sasa ndiye mtu anayejadiliwa zaidi hapa Dodoma kwa sasa kutokana na tukio hilo.
Updates...........
Hamadi Rashidi katika mahojiano na MWANANCHI JUMAPILI amekiri kuwashawishi wajumbe hao ili waipitishe rasimu ila amekana kuwanunua "Ni ushawishi wangu tu ili kuwakomoa CUF" alijigamba Rashidi.
Ila ukweli ni kuwa wajumbe hao waliahidiwa kiwango hicho cha fedha.
Pia wapo wa kura za siri waliopiga kura za 'HAPANA' takribani wajumbe 17 ingawa Hamadi Rashidi anatudanganya kuwa ni yeye aliwashawishi wapige kura za siri na wote walipiga za 'NDIYO' na anadai eti baada ya kupiga walikuwa wakimuonyesha ili athibitishe! Huu ni uongo wa wazi kabisa!!!!!