Tukitala kuishinda ccm lazima kuwe na mageuzi makubwa ndani ya vyama vyetu vya siasa, viongozi wengi wa vyama hivi wamekuwa madarakani kwa muda mrefu, na wameshindwa kutufikisha watanzania tunapo pataka, wametengeneza safu za utawala ambao unawazuia wengine kuwapinga na kuweka changamoto.
Lengo la chama chochote cha upinzani ni kutawala nchi, lakini inapofikia viongozi wa vyama hivyo wanausaidia chama tawala kuendelea kutawala, inakuwa hakuna haja tena ya kuwa na vyama vya upinzani. Kama wakatokea watu ndani ya vyama vyetu, wakataka mabadiliko wanaoneka ni waasi, bado tunaunga mkono kuwajibishwa kwao kwa kisingizio kuwa vyama vinalinda katiba, wakati ukweli ni kuwa viongozi wanalinda masilahi yao binafsi.
Kwa suala la David na la Rashidi, tumekuwa tukitoa mchango kiushabiki zaidi, badala kuangalia ukweli wa mambo, kukubali na kunyamaza kimya si utii bali ni uoga, wale wanao mshauri Davidi kuomba msamaha kwa viongozi wake ni sawa na kumfundisha uoga, haitasaidia kitu kama akiomba msamaha kwa kuwa moyo wake unataka mabadiliko.
Kama tukisema David au Rashidi wamevunja katiba ya vyama vyao, mbona sisi viongozi wengi tu waupinzani tunavunja katika ya nchi katika mambo mengi, lakini kwa kuwa lengo letu ni moja, kuleta mabadiliko ndo maana tunakuwa na moyo wa kiujasiri, kama MB David kavunja katiba ya chama chake akafukuzwa, basi na wale wabunge wanovunja katiba ya nchi kwa madai ya kudai haki itabidi wafungwe kabisa.
Katiba zote zimeandika na kutungwa na watu kwa lengo la kulinda masilahi ya kiuongozi na kiutawala, ukitaka mabadiliko lazima kwanza uivunje hiyo katiba.
Kwa kumalizia, katika mfumo huu tulio nao katika vyama vyetu vya siasa, itakuwa ngumu sana ku defeat CCM. CCM ni chama kikongwe, kina mikakati mingi sana na hila nyingi za kuendelea kutawala, hata kuweka mapandikizi na kuwanunua baadhi ya wanasiasa wa upinzan, ili kuweza ku defeat CCM inabidi kwanza kufanya mapinduzi makubwa katika mifumo yetu ndani ya vyama vyetu vya upinzani, lengo letu wote liwe ni moja, kufanya mabadiliko katika nchi na sio kutaka madaraka.