Hamad Rashid aomba radhi...

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,142
13,216
[h=1][/h]Written by Elbattawi // 21/12/2011 // Habari // No comments

BAADA ya Chama cha NCCR-Mageuzi kumtimua uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David kafulila, kutokana na shutuma alizotoa dhidi ya Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia, upepo wa kisiasa unaonekana kubadilika ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), baada ya wanachama kadhaa waandamizi kudai kwamba Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed, ameamua kumwangukia Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.
Kama Kafulila ambaye amekuwa akisema Mbatia ameua NCCR-Mageuzi, Hamad Rashid naye yumo katika mgogoro mkubwa na Maalim Seif, akitaka kugombea nafasi ya ukatibu mkuu ili kukijenga upya chama chao.
Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika ndani ya CUF vililiambia gazeti hili kuwa baada ya kuona yaliyomkuta Kafulila – kupoteza uanachama na ubunge – Hamad Rashid ametuma ujumbe mzito kwa Maalim Seif kumwombea radhi.
Miongoni mwa wajumbe waliotumwa kumwangukia Maalim Seif kwa niaba yake ni masheikh na wazee saba wanaoheshimika.
Habari hizo zinasema hata hivyo, Maalim Seif alitilia shaka ujumbe wa watu hao, akasema anashangazwa na kauli zinazoendelea kutolewa na Hamad Rashid hadharani na katika vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo ndani ya CUF, mbali na hatua ya NCCR-Mageuzi kumfukuza Kafulila uanachama, na kwa mantiki hiyo akapoteza ubunge, uamuzi wa Hamad Rashid umetokana pia na kauli ya Maalim Seif alipozungumza na vyombo vya habari majuzi, akimtaka Hamad Rashid akumbuke yaliyowatokea viongozi wengine waandamizi kina James Mapalala na Naila Jiddawi.
Huku akijaribu kuepuka kuzozana na Hamad Rashid magazetini, Maalim Seif alisema uamuzi wowote dhidi ya Hamad Rashid, ambaye wanachama na viongozi kadhaa wamemuita muasi, utachukuliwa ndani ya vikao vya chama.
Tayari Hamad Rashid amejiapiza kumng’oa Maalim Seif katiba nafasi ya ukatibu mkuu uchaguzi utakapofika. Na ametishia kwamba iwapo chama hicho kitamfukuza uanachama kwa sababu hii, yupo tayari kuanzisha chama kingine akishirikiana na viongozi na wanachama wengine waandamizi waliochoshwa na uongozi wa Maalim Seif.
KAULI YA HAMAD RASHID
Hata hivyo, alipohojiwa na gazeti hili jana kuhusu taarifa za yeye kumwangukia Maalim Seif, Hamad Rashid alikataa katakata, akisema hawezi kufanya hivyo.
Alikana kutuma ujumbe huo wa wazee saba kumwangukia Maalim Seif kumaliza tofauti zao, huku akiziita taarifa hizo kuwa za kizushi.
Hamad Rashid alisema tangu mzozo kati ya viongozi hao uanze, hajawahi kuonana na Maalim Seif wala hajamtuma mtu kuomba radhi kama inavyovumishwa sasa.
Alisema kuwa hana mpango huo wala hafikirii kuchukua hatua ya kumwomba mtu yeyote msamaha kwa vile anajua hana kosa na aanachokisimamia ni haki yake ya msingi na ya kikatiba.
“Naweka wazi kuwa huo ni uongo wa waziwazi ambao unalenga kuwapotosha na kuwachanganya wananchi na hasa wanachama wa CUF.
“Sina mpango na wala sifikirii kwenda kumwomba radhi Maalim Seif wala kiongozi yeyote kama wanavyotaka kuwaaminisha wananchi,” alisema Hamad wakati alipohojiwa na Tanzania Daima kwa njia ya simu.
Bila kusita, mbunge huyo alimtuhumu Ismail Jussa Ladhu kuwa ndiye anayeeneza uzushi huo kwa lengo na nia anayoijua yeye, kwa madai kuwa ni hulka yake ya siku zote kutoa kauli za kuzua.
“Kama habari mnazoniambia ni za kweli, basi anayeeneza uongo huo ni Jussa, maana ni hulka yake hata kule bungeni aliwahi kusema uongo akaambiwa athibitishe lakini akashindwa.
Hamad Rashid aliongeza kuwa hana sababu ya kutaka vikao vya kuombana msamaha na wala haogopi kutimuliwa ubunge kwa sababu anajua anachokitetea na kinaungwa mkono na viongozi na wanachama wengi ndani ya CUF.
Mzozo baina ya viongozi hao wawili waandamizi ulisababisha vurugu kubwa na mapigano kati ya wanachama wanaowaunga mkono viongozi hao.
 
huyu ni wa kufukuza tu ..nilikuwa namheshimu sana kumbe ana tamaa sana ya madaraka ..nonsense
 
Yaaah, kuna mwanazuoni mmoja aliwahi kusema nanukuu........"Waacheni wafu wakazike wafu wao"
 
Nitashangaa kama hawatamfukuza. i can see impotance ya Hamad kuachia ukatibu mkuu lakini sio mbeleko ya uhaini wa Hamadi.
 
Wanazuoni walisema pia ''kama huna uwezo wa kupambana na adui yako PATANA NAE TU''H.Rashidi machale yamemcheza kaona hii ngoma ni nzito bora aachane nayo.
 
BAADA ya Chama cha NCCR-Mageuzi kumtimua uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David kafulila, kutokana na shutuma alizotoa dhidi ya Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia, upepo wa kisiasa unaonekana kubadilika ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), baada ya wanachama kadhaa waandamizi kudai kwamba Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed, ameamua kumwangukia Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad.
Kama Kafulila ambaye amekuwa akisema Mbatia ameua NCCR-Mageuzi, Hamad Rashid naye yumo katika mgogoro mkubwa na Maalim Seif, akitaka kugombea nafasi ya ukatibu mkuu ili kukijenga upya chama chao.
Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika ndani ya CUF vililiambia gazeti hili kuwa baada ya kuona yaliyomkuta Kafulila – kupoteza uanachama na ubunge – Hamad Rashid ametuma ujumbe mzito kwa Maalim Seif kumwombea radhi.
Miongoni mwa wajumbe waliotumwa kumwangukia Maalim Seif kwa niaba yake ni masheikh na wazee saba wanaoheshimika.
Habari hizo zinasema hata hivyo, Maalim Seif alitilia shaka ujumbe wa watu hao, akasema anashangazwa na kauli zinazoendelea kutolewa na Hamad Rashid hadharani na katika vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo ndani ya CUF, mbali na hatua ya NCCR-Mageuzi kumfukuza Kafulila uanachama, na kwa mantiki hiyo akapoteza ubunge, uamuzi wa Hamad Rashid umetokana pia na kauli ya Maalim Seif alipozungumza na vyombo vya habari majuzi, akimtaka Hamad Rashid akumbuke yaliyowatokea viongozi wengine waandamizi kina James Mapalala na Naila Jiddawi.
Huku akijaribu kuepuka kuzozana na Hamad Rashid magazetini, Maalim Seif alisema uamuzi wowote dhidi ya Hamad Rashid, ambaye wanachama na viongozi kadhaa wamemuita muasi, utachukuliwa ndani ya vikao vya chama.
Tayari Hamad Rashid amejiapiza kumng’oa Maalim Seif katiba nafasi ya ukatibu mkuu uchaguzi utakapofika. Na ametishia kwamba iwapo chama hicho kitamfukuza uanachama kwa sababu hii, yupo tayari kuanzisha chama kingine akishirikiana na viongozi na wanachama wengine waandamizi waliochoshwa na uongozi wa Maalim Seif.
KAULI YA HAMAD RASHID
Hata hivyo, alipohojiwa na gazeti hili jana kuhusu taarifa za yeye kumwangukia Maalim Seif, Hamad Rashid alikataa katakata, akisema hawezi kufanya hivyo.
Alikana kutuma ujumbe huo wa wazee saba kumwangukia Maalim Seif kumaliza tofauti zao, huku akiziita taarifa hizo kuwa za kizushi.
Hamad Rashid alisema tangu mzozo kati ya viongozi hao uanze, hajawahi kuonana na Maalim Seif wala hajamtuma mtu kuomba radhi kama inavyovumishwa sasa.
Alisema kuwa hana mpango huo wala hafikirii kuchukua hatua ya kumwomba mtu yeyote msamaha kwa vile anajua hana kosa na aanachokisimamia ni haki yake ya msingi na ya kikatiba.
“Naweka wazi kuwa huo ni uongo wa waziwazi ambao unalenga kuwapotosha na kuwachanganya wananchi na hasa wanachama wa CUF.
“Sina mpango na wala sifikirii kwenda kumwomba radhi Maalim Seif wala kiongozi yeyote kama wanavyotaka kuwaaminisha wananchi,” alisema Hamad wakati alipohojiwa na Tanzania Daima kwa njia ya simu.
Bila kusita, mbunge huyo alimtuhumu Ismail Jussa Ladhu kuwa ndiye anayeeneza uzushi huo kwa lengo na nia anayoijua yeye, kwa madai kuwa ni hulka yake ya siku zote kutoa kauli za kuzua.
“Kama habari mnazoniambia ni za kweli, basi anayeeneza uongo huo ni Jussa, maana ni hulka yake hata kule bungeni aliwahi kusema uongo akaambiwa athibitishe lakini akashindwa.
Hamad Rashid aliongeza kuwa hana sababu ya kutaka vikao vya kuombana msamaha na wala haogopi kutimuliwa ubunge kwa sababu anajua anachokitetea na kinaungwa mkono na viongozi na wanachama wengi ndani ya CUF.
Mzozo baina ya viongozi hao wawili waandamizi ulisababisha vurugu kubwa na mapigano kati ya wanachama wanaowaunga mkono viongozi hao.
KAULI YA JUSSA
Juhudi za kumtafuta Jussa zilikwama, baada ya simu yake ya mkononi kuita mara nyingi bila kupokewa.

Source: Tz daima
 
Hamad Rashid = ukatibu mkuu wa chama chaake CUF
David Kafulila = Uwenyekiti wa chama chake (kilichokuwa chama chake?) NCCR......

So kama HR naye atafukuzwa, hicho chama kipya kitakuwa na Mwenyekiti na Katibu Mkuu tayari!
Ikizingatiwa historia ya ushirikiano wao kwa matukio ya bungeni ni wazi sana hawa mabwana wanapikika na wataiva
 
Acheni uchochezi.

ya ng'oswe aachiwe ng'oswe mwenyewe. Kwani naamini kuna taratibu na utamaduni wa kujadili mambo pasi na kupiga kelele nje.
 
Back
Top Bottom