Hamad Rashid aing'arisha Tanzania kimataifa..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamad Rashid aing'arisha Tanzania kimataifa.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Oct 25, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180  Mbunge wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani Mhe. Hamad Rashid Mohamed ameteuliwa na kamati tendaji ya chama cha Mabunge duniani (IPU) kuwa mjumbe wa kamati ndogo ya ukaguzi wa ndani kwa mahesabu ya mwaka 2013 ya chama hicho.

  Uteuzi huo ulifuatia pendekezo la umoja wa Mabunge ya Afrika lililowasilishwa na katibu mkuu wake Koffi N'Zi tarehe 22 Oktoba, 2012 kufuatia kikao cha wajumbe wa umoja wa Mabunge ya Afrika kumchagua Mhe. Hamad kuwakilisha Afrika kuwania pendekezo hilo mbele ya kamati tendaji ya chama hicho.

  Mhe. Hamad Rashid Mohamed, hii ni mara ya pili kuiwakilisha Tanzania na Afrika katika kamati mbalimbali za IPU ambapo mwaka jana katika Mkutano uliofanyika Mjini, Benn, Uswis, alichaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya IPU cheo ambacho anakitumikia hadi hivi sasa.

  Katika kamati hiyo ya ukaguzi wa ndani, Mhe. Hamad Rashid atafanya kazi pamoja na mjumbe mwingine aliyeteuliwa Mhe. Duarte Pacheko kutoka Ureno, ambapo wanatarajia kutoa taarifa ya kazi yao mwaka 2014 katika mkutano mkuu wa IPU

  JIWE WALILOKATAA WAASHI LINAPOKUWA JIWE KUU LA PEMBENI
   
 2. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,309
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Mwenyezi mungu amuongoze vyema.
   
 3. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #3
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  CUF watalikumbuka Jembe lao hili
   
 4. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #4
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Ingawa aliwanyoosha akina Dr Slaa enzi alipokuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni. labda huko anakutana na wajanja zaidi yake
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Oct 25, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,814
  Likes Received: 5,133
  Trophy Points: 280
  ..Hamad Rashid hataki kupumua na muungano wa mkataba??
   
 6. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #6
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  anavyofaidika na muungano huyo hataki hata kusikia issue za akina Maalim seif na Jusa
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hapa ndipo unapoonekana mtu wa ajabu.Mambo ya kuwaanyoosha Dr Slaa yanahusika vipi hapa.Kitu kidogo tu kinaharibu hoja yako yote.
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  What goes around, comes Around...
  BEWARE !!!
   
 9. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #9
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  usijali sana ukitaka kuniona mtu wa ajabu poa tu. lakini ukweli ndio huo

  alipokuwa kiongozi wa upinzani bungeni wale mawaziri vivuli wote walikuwa wakipata tabu sana wanapoandaa bajeti zao na hata wakati mwingine walipaswa kutoa pesa zao mfukoni bila kupata msaada wowote wa Ofisi ya kiongozi wa upinzani wakati bajeti ni ya kambi ya upinzani.

  Hili Dr Slaa hatasahau walivyokuwa wakifanyiwa na huwa anasema kwa uwazi hata kama wewe hupendi kulisikia.
   
 10. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,224
  Likes Received: 1,071
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu jamaa ni Mbunge kupitia chama gani?
   
 11. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Congrats Hon. Hamad Rashid

  Nilikuwa namkubali sana wakati akiwa KUB lakini baada ya kuikosa nafasi ile akaporomoka kwenye ubinafsi na choyo dhidi ya CDM. Kwa ujumla huwa ni mchakapazi mzuri na mjenga hoja mzuri.
   
 12. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Labda atatulia huyo mpenda madaraka
   
 13. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Where is Mr Mangi Masta?
   
 14. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kupitia CUFU mkuu!!! Bunge letu ninamtuambua kama mbunge halali wa CUF kama ilivyo kwa Kafulila na NCCR Mageuzi!!! Utaziweza SI HASA za nchi hii!!!?
   
 15. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #15
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Tunasubiri maamuzi ya jaji kama atamfunga jela makamu wa rais Maalim seif na Mtatiro wake maana dalili zaonyesha kuwa na hatia na kilichobaki ni kuangalia impact yake itakuwa nini wakifungwa maana kosa la kudharau mahakama halina faini, ni jela tu. Hamad kweli kiboko
   
 16. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2012
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Hongera Bw Hamad Rashid, mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CUF, na pia mlezi wa chama cha ADC.
   
 17. M

  Mgelukila JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siyo mwadilifu kivile, anavimeo kibao anashindwa kulipa, anatoa cheques hewa, ukimpigia simu hapokei anaishia kuzima simu na kuhama line za simu. Hata ofisi kahamisha upanga hataki kutoa ushirikiano.
   
 18. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Ameing'arisha vipi?
   
 19. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Ajihadhari na Mulugoism.
   
 20. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,401
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Ok anaiwakilisha Tanzania. Muungano ukivunjika ataiwakilisha nchi gani?
   
Loading...