Hamad Rashid abwagwa kortini

WOWOWO

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2011
Posts
599
Reaction score
457
Kutoka mujibu wa Julius Mtatiro...


My Take
Nini hatma ya Hamad Rashid kisiasa maana ni wazi upepo si mzuri kwake?
Je ni wakati sasa wa CDM kufikiria kumpa nafasi Mh. Rashid ili kuendelea kujijenga visiwani Zanzibar baada ya kuwa na makada wa aina ya Profesa Safari?

Ni wazi mchango wa Hamad Rashid katika kuleta mageuzi nchini si wa kubeza. Aliweza kuiongoza kwa ushupavu kambi ya upinzani bungeni 2005-2010 na ikaleta matunda mazuri. Pamoja na kuhusishwa na ADC (hakuna ushahidi) anaweza kupewa nafasi CDM?

Tujadili hoja, bila matusi
 
Tuwaache wafu wazikane, maana kilaza Mtatiro hata point zake hatuzioni,
zaidi ya kuone tarehe ya kesi 28/01/2013 na pole ya msiba
 
WOWOWO Hivi Hamad na Mtatiro wana utafauti wowote? Labda Sura lakini si wote wako kwenye Payroll ya CCM kuuvuruga UPINZANI? TAFAKURI
 
Last edited by a moderator:
Chama pia kinatoa pole kwa mhe. Hamad Rashid kwa kufiwa na mkewe mdogo jana, tutashiriki katika kutoa pole na mazishi pia. Tunaamini haya ya kimahakama yana nafasi yake na ya kibinadamu hayakwepeki.
Nimependa hii sana.. Juu ya magomvi na mitafaruku ila kwenye miciba na matatizo tofauti na magomvi yawekwe pembeni.. Pole HR kwa kufiwa na mke wake.. Mungu ampe ustahimilivu na subira kipindi hiki kigumu kwake...
 
Haya Bwana Mkubwa! Wewe unasema kuwa umefurahishwa na uamuzi wa mahakama au unafurahishwa na kifo cha mke wa mtu? Mambo ya kushiriki kuzika au kutozika marehemu kwa hicho chama chako ina nafasi gani kwa wana jamii kuchangia hoja yako?

Naona cha msingi hapa ni mleta hoja hii kutaka kutafuta maneno kwa wana CDM. Kweli hali ni mbaya huko CUF.
 
Julius Mtatiro, tafadhali nisaidie majibu ya maswali haya:-

Nani ka kwakwambia kwamba CDM wanamtaka Hamad kuimarisha chama visiwani?
Mambo ya CDM yanakuhusu nini wewe Kama kiongozi mkubwa wa chama Chako?
Huoni Kama unapoteza muda kwa kitu ambacho hakikuhusu?
 
Last edited by a moderator:
His rightful place is in ADC; anashabihiana nao kwa mawazo, maono na historia.
 
Hamad Rashid ni mwanasiasa uchwara mwenye uroho wa madaraka. Hatumtaki huku CHADEMA. Tunataka wanasiasa wenye bright vision and mission kuhusu chama na nchi. Namshauri ajiunge rasmi na CCM kwani huko ndio kuna wanasiasa wa aina yake.
 
mnafiki mkuibwa huyo aende ADC SASA TUONE.SI KIMESAJILIWA TAYARI?
 
Mwanzoni Alivuruga ccm akatimuliwa, kavuruga CUF akatimuliwa, Hamuoni huyu mtu ana CV yenye Utata?? kwani CDM ni jalala?
 
CDM mnangojea kupokea viongozi wanaotemwa? Viongozi huandaliwa, mkingojea kupokea makombo mtaishia shimoni!

Hamad Rashid, Safari na wenzao umaarufu wao umekwisha ndani ya cuf sasa kama nyinyi chadema mna uwezo wa kuwasafisha na kuwajenga upya mnakaribishwa.
 
Ndugu Julius kwa jinsi alivyoandika hii habari yake anaonekana anafurahi sana kwa Hamad kuanguka kisiasa, siri ya furaha hiyo anaijua mwenyewe, kijana Mtatiro simtofautishi na kijana Nape kwa jinsi wanavyopenda kuwafurahisha kisiasa wakubwa zao hata katika mambo ya kipuuzi......

HR ni mwanasiasa mkongwe ndani ya chama cha CUF anaponzwa na uthubutu wake wa kuwahoji viongozi wakuu, Mtatiro CUF umeijua juzi kati we tumika halafu uone hao wapemba watakupa medali gani.
 
Sio mpemba tu hiyo ni sheria ya uislamu kma ukiwa na uwezo unaweza kuoa hadi wake wa4
 
Pole sana Hamadi Rashid kwa msiba wa mke wako.
 
Nadhani Hamadi Rashid hahitaji kujiunga na chama kingine maana ana chama kingine tayari ambacho ameishakisajiri, ni mlezi wa chama cha ADC. Mmesahau?

Quality
 
Binafsi ningefurahi kama HR angejiunga na CDM, Tungekua rtumepata mshirika mzuri ktk siasa za Znb na wale waumini wa siasa za kidini ambao wamekua wakiongezeka sana ktk siku za karibvuni
 
maswala ya kisiasa yanabadilika ka bahari si kitu cha kuaminika sana
Hata mulete Malaika
kutoka mbinguni CHADEMA ndani ya Zanzibar hamukubaliki. Chama
kinaonekana na UDINI wa wazi wazi, CHADEMA kukubalika Zanzibar ni sawa
na Muislamu kula nyama HARAMU ya nguruwe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…