Hamad: Lipumba anajua kabisa mkutano wake si halali, hautambuliwi na Mahakama.

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,274
47,339
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema hawautambui mkutano huo kwa sababu una zuio la Mahakama Kuu.

Akizungumza na Mwananchi Jumanne Machi 12, 2019, Maalim Seif amesema, sisi hatuna uwezo wa kuuzuia lakini kama jeshi la polisi likitaka linao uwezo huo.

“Ni kama mchezo wa kuigiza kuhusu suala hili, kama polisi ina nia ya dhati ya kuzuia wale hawawezi kufanya lolote lile. Utafanyaje mkutano wakati kuna zuio tena la Mahakama Kuu? Alihoji Maalim Seif.

“Siyo mantiki yoyote kwa polisi kuanza kuzungumza na viongozi wa CUF wa upande ule wakati suala lipo wazi kabisa. Nawaambia msimamo wetu upo pale pale mkutano huu hatuutambui kabisa kwa sababu ni haramu,” amesema Maalim Seif.

CUF upande wa Profesa Ibrahim Lipumba unafanya mkutano mkuu jijini Dar es Salaam ambapo polisi wa Ilala umeuzuia mkutano huo lakini agizo hilo halikutekelezwa na mkutano uliendelea.
 
Ninachokiona ktk hili sakata, ni wazi maalum atakwenda kupotezwa KISIASA pamoja na kwamba Mahakama ipo upande wake. Lipumba na kundi lake wameshapeta hapa na Leo ndio mkutano Mkuu. Ni vema Wabunge na Maalim wawe wapole waende kikaoni Hata km ni kuwaenjoy tu Lkn mwishowe timu Lipumba watafurahi siku mbili kwamba ni washindi na mwishowe cut itarejea ilengangari.
Hata hivyo siwaungi mkono wanaobeza kwamba UKAWA haikuwasaidia. Huku ni kukosa busara na shukrani . Tuwatakie mwisho mwema watoke wakiwa wamoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utawala wa jiwe unajichafua wenyewe halafu lawama zinaelekezwa Kwa TAL

Sidhani kama CUF Self wana mpango huo. lengo la serikali ni kuona CUF ikifa.
 
Back
Top Bottom