GreaThinkers,
Kuna Tetesi ya kutolewa hadharani matokeo ya Uchaguzi 2010 visiwani ambapo kwa tetesi zilizoenea mdogo mdogo ni kuwa Maalim(CUF) alimshinda Shein(CCM) kwa tofaouti ya kura zisizopungua elfu Ishirini ivi(20,000)
Baada ya kikao cha siri baina ya wakubwa hao, kura zilirekebishwa na ule msimamo wa CUF wa kuwa na Serikali tatu ukafia pale pale. Hakuna hakika kama Katiba ya CUF pia imerekebishwa hapa.
Tetesi zinasema CUF inaelekea kumegeka na kuwa kundi kubwa la Hamad ni bara na Unguja huku CUF ya Pemba inamuunga mkono Seif.
Hamad anaweza kuanzisha Chama chake ilaTetesi zinasema pia kuwa anataka kuunga mkono chama kimojawapo chenye nguvu Tanganyika
Je ni kweli akijiunga na chama chenye nguvu Tanganyika atafanikiwa?
Je akianzisha Chama chake atafanikiwa?
Nini maoni yako?
Barubaru,Je unamfahamu Hamad Rashid? au unarukia pasi na kumjua vyema hamad Rashid.
Kwa kukudondolea kidogo tu. Huyu si mtu wa kujichanganya na watu japo binafsi ana akili sana kiutendaji na ndio maana wanaomfahamu sio tu unguja na pemba bali mpaka hata Bara hajawa maarufu wa kuweza kuanzisha chama au hata kupewa nafasi ya juu ya kisiasa.
Huo ni ufupi tu.
Barubaru,
Itakuwa Too late kufuta kauli yako huyu bwana akianzisha chama chake.
Je umeskia tamko la CUF Dar?
Je Umeskia Tamko la CUF Mwanza?
Think
Natamani nisikie na CHADEMA, mmoja atangaze kumng'oa Mbowe au Slaa ili tuone hawa wanaojiita wanademocrasia kama wamekomaa au wanatuzuga tu
Mdau inaonekana unayajua mengi sana kuhusu hili sakata,hebu mwaga mchele utuamshe nasisi tuliopo usingizini!Kumbe kuna system ya magamba ndani yake?halafu kweli maana hawa jamaa wote Maalim na Hamad wametokea magamba!!Kitu ambacho wengi wetu wanashindwa kuelewa ni kuwa, system ipo kazini kuhakikisha kuwa CUF hawapati majority ya kura za Zanzibar 2015. Seif na Hamad wote wapo kwenye system na hii ni assignment yao ya sasa. Divide and Rule.
Natamani nisikie na CHADEMA, mmoja atangaze kumng'oa Mbowe au Slaa ili tuone hawa wanaojiita wanademocrasia kama wamekomaa au wanatuzuga tu
hr ndo amekwisha. Cuf itabaki na itaendelea na harakati za kisiasa. Kwa wenye akili timamu na kumbukumbu za kutosha wanajua kwamba kwa tz cuf ndo chama pekee ambacho kimekumbana na mikiki mikiki mikubwa bila kutetereka huku kikiendelea na misimamo ya kulinda sera na katiba ya chama bila kujali uwezetu au uveterani. Ni somo tosha kwa wasiopenda kuwajibika au kutumia sheria zilizopo kuwajibishana. Gamba limeshinda kuvuliwa kwa hofu ya kugawa chama - hakuna kitu kama hio ndani ya cuf-sharia ni msumeno. Leo hr na wenzake watasema mengi but now they are out of the system. Msumeno umekereza nguzo walioegemea imekatika wemeanguka na hawatoinuka kisiasa. Kuna inspector mmoja aliwahi kuonesha aina zote za silaha (za kienyeji) ili kuipakazia cuf ila yuko wapi sasa. Kuna kiongozi mmoja alikua akiwakebehi, kuwaadhibu na kuwadhalilisha cuf na viongozi wao yuko wapi sasa? Kidombooooooo hata macho hayana nuru! Yuko wapi yule kijana alieisaliti cuf mkunazini na kuhamia ccm kama mpiga uongo-propaganda? Karejeshwa znz kwa kigari sasa anatembea kwa mkongojo! Cuf imesimama kwa misingi imara na kitadumu. Sheria ni msumeno. Seif anasimamia sheria za chama. Ana udhaifu kama binadamu wengine ila hao kina hr wanashindwa kuleta ushahidi wowote wa kukiuka au kuvunja taratibu za chama kama seif (kama amewahiufanya hivyo ni kupitia vikao vya chama na hapo inakua sio maamuzi yake bali ni maamuzi ya chama). Hr and allies watafute biashara wafanye wameshindwa kuonesha uvumilivu wa kisiasa walitaka kwa nguvu ila wamepiga ngumi ukuta...
Je unamfahamu Hamad Rashid? au unarukia pasi na kumjua vyema hamad Rashid.
Kwa kukudondolea kidogo tu. Huyu si mtu wa kujichanganya na watu japo binafsi ana akili sana kiutendaji na ndio maana wanaomfahamu sio tu unguja na pemba bali mpaka hata Bara hajawa maarufu wa kuweza kuanzisha chama au hata kupewa nafasi ya juu ya kisiasa.
Huo ni ufupi tu.
Mimi nimesikia Askari polisi walivyomsifia kwa kutetea maslahi Yao na umahiri wake katika bunge pamoja na kuwaombea na kufanikisha msaada Ujenzi wa nyumba za Kilwa rd,jeshi la magereza kujitosheleza kwa chakula,kutekeleza magereza kujua Shida za wafungwa,hadi kushauri waanzeshe miradi I takao wapa kipato wamalizapo kifungo.pia nilisikia alivyo kuomba kim il sung na kusaidia mradi mkubwa wa uwanja wa Michezo gombani,nyumba za polisi raha wete .haya Ni machache tu,lakini tujuilize mwalimu kwanini alimpenda na kumuamini sana HAMAD.nafikiri Ni uzalendo wake. Ya karibuni Ni umahiri wake alivyoweza kuiunganisha kambi ya upinzani bungeni, jambo ambalo Mbowe hajaweza.hivi hamad rashid ameisaidia nini tanzania kama kiongozi,.