Halotel mmeanza kupuyanga sasa!

Halotel mmeanza kupuyanga sasa!

Tuliwapokea vyema na speed ya internet yenu ilitubamba ila kwa sasa naona mmeelemewa na mzigo aisee. Yaani hata Live streaming tu ni shida, tena huu mwezi ndio kabisaaa!!

Kupost tu hii thread, imenichukua 3times retrying. Bora hata nirudi voda kwa wapigaji maana mitandao mingine ndio wababaishaji tu.

Wameshawapata Wateja wa kutosha hivo wamesharidhika
 
TTCL wamejaa ukiritimba nilinunua line yao nilipo iweka kwenye simu yangu ikawa haisaport Internet nilipowapigia wakaniambia hadi nirudi head office ili waifanyie configuration phone yangu ndio isaport internet sasa mda huo Mimi napata wapi line nilisha tupa na sihiitaji tena Huduma za Bibi
Tatizo ni kwamba watu tunaongea nao kupitia customer care hawajui technical issues. Jana nlikuwa naongea na mmoja wa halotel namweleza kuwa pamoja na kuwa internet inasoma 3G Lkn siwezi kufanya chochote na internet yao tofauti na tgo ambayo ikisoma 3G inapeleka though kuipata iyo 3G ni ishu. Jamaa akaniambia niende kwenye setting nifanye restoration ya settings. Nkamuuliza unamaanisha nifute vitu vyangu vyote?akasema ndio, nkamuuliza ndovyo unavyowaambia wateja wote wenye tatizo km hili?akaanza kubabaika. Nkajua tu anafanya kwa kukisia. Kwaiyo sometimes ukiona wa kwanza anazingua inapiga tena (km una muda lakini) unaweza kumpata atakayekupa maelezo tofauti na yakakusaidia
 
Back
Top Bottom