Halotel mmeanza kupuyanga sasa!

lossoJR

JF-Expert Member
Oct 11, 2012
2,711
2,383
Tuliwapokea vyema na speed ya internet yenu ilitubamba ila kwa sasa naona mmeelemewa na mzigo aisee. Yaani hata Live streaming tu ni shida, tena huu mwezi ndio kabisaaa!!

Kupost tu hii thread, imenichukua 3times retrying. Bora hata nirudi voda kwa wapigaji maana mitandao mingine ndio wababaishaji tu.
 
Hawa wameshakua maboya cku moja niliwapigia nikawauliza kulikoni wakanijibu utumbo cna hamu nao hao
 
Nimeingia mkenge leo kwa kujiunga na kifurushi cha elfu 10. Mwanzo nilikuwa natumia intaneti ya voda na iko powa kabisa,baada ya kusoma maoni watu mitandaoni kwamba halotel ndo kiboko ya wote ndio nikaona nami niende huko. Niliyo yakuta huko ni madudu tu. Nimeshindwa kuona hata mechi live. Baada ya kurudishia voda naona mambo powa kama zamani na voda intanet. Hallotel ni baba moja na airtell kwa intranet
 
Mkuu yani mm nipo chini ya mnara wao kabisa lkn wako ovyo kweli!

Ila bado naiona halotel ni kiboko kulinganisha na hawa kobe wengine!
 
Mm binafsi hawa jamaa halotel wamenisaidia kiasi flani. Coz eneo nililopo kuna bonde ivi na mnara wa tigo ipo just few meters kutoka hapa lkn internet yao ni ya hovyo kuliko hovyo yenyewe lkn nlipojaribu halotel japo hata mnara wao siuoni naona inasukuma kidogo though kasi yao pia hairidhishi Na km wanapita kumu basi wanaona wateja wanayoyaandika
 
Mitandao ya Tigo na Voda hivi sasa inamilikiwa na wahindi kwa hiyo mwendo ni maumivu tu kwenye bando alafu hao TCRA ndio hovyo kabisa wamerudisha nyuma juhudi za Rais mstaafu kuweka mkonga wa taifa ili watu wapate huduma ya internet kwa urahisi na kasi
 
TTCL wamejaa ukiritimba nilinunua line yao nilipo iweka kwenye simu yangu ikawa haisaport Internet nilipowapigia wakaniambia hadi nirudi head office ili waifanyie configuration phone yangu ndio isaport internet sasa mda huo Mimi napata wapi line nilisha tupa na sihiitaji tena Huduma za Bibi
 
Bora nyie huko
Huku kwetu tuliambiwa hatuna smartphone hivyo hawawezi kuwezesha internert yenye kasi.Aaaaa,..upuuuzi.
 
Back
Top Bottom