Halotel mmeanza kupuyanga sasa!

Halotel mmeanza kupuyanga sasa!

Tuliwapokea vyema na speed ya internet yenu ilitubamba ila kwa sasa naona mmeelemewa na mzigo aisee. Yaani hata Live streaming tu ni shida, tena huu mwezi ndio kabisaaa!!

Kupost tu hii thread, imenichukua 3times retrying. Bora hata nirudi voda kwa wapigaji maana mitandao mingine ndio wababaishaji tu.
Mimi nilidhani simu yangu mbovu
 
Mkuu line ya TTCL unayo au umewahi kuijaribu ? Kiukweli TTCL wapo vizuri huwezi kuifananisha na Halotel kwa sasa ambao mb zinavyokata huwezi kuelewa na kasi taratibu imeanza kufifia
eeeh mkuu hao Ttcl ndio sitaki wasikia kabisa maana ni matapeli wa kutupwa,nilinunua line yao juzi lakini walichonifanya baada ya mita kadhaa nikaambulia patupu
 
Jamani ttcl 4g ni zaidi ya noma kwenye speed, au connect na fiber ndio utajua mwisho wa maneno...hakika ttcl ni baba lao
Hao ttcl saizi spidi lazima iwe kubwa maana hawana wateja wengi si mnakumbuka halotel wakati inaanza kila mtu aliisifia saizi majanga tu
 
eeeh mkuu hao Ttcl ndio sitaki wasikia kabisa maana ni matapeli wa kutupwa,nilinunua line yao juzi lakini walichonifanya baada ya mita kadhaa nikaambulia patupu
TTCL zinashika vizuri kwa cmu zenye uwezo mkubwa wa internet kasi yao wanajitahidi.
 
Hawafai kabisa, nahisi hata bunde za internet wanatuibia. Hazichukui muda tayari zimekwisha tofauti na zamani.
 
Tuliwapokea vyema na speed ya internet yenu ilitubamba ila kwa sasa naona mmeelemewa na mzigo aisee. Yaani hata Live streaming tu ni shida, tena huu mwezi ndio kabisaaa!!

Kupost tu hii thread, imenichukua 3times retrying. Bora hata nirudi voda kwa wapigaji maana mitandao mingine ndio wababaishaji tu.
Usije ukaenda Tgo speed ya Kobe
 
Back
Top Bottom