Halotel janga jingine

Hata sikuelewi halotel ilivyo poa mpaka vijijni mtandao upo
 
Daah watanzania sisi tuna shida sana.Nimesikitika sana na hii habari yako.
 
aah wapi halotel khabari nyingne wewe......tatizo umezoea wale machakavu unatafta attention ya watu pole sana sijutii kutumia halotel
 
Sikuhizi wameanza mchezo wa kunidisconnect kila baada ya muda fulani. Speed nayo sio poa kama ilivyokuwa miezi kadhaa iliyopita.
 
Ukweli ni kuwa kila mtandao kuna maeneo ambayo unakuwa na nguvu katika internet.

Binafsi nikiwa Posta DSM napata internet ya mitandao yote bila wasi kwa sababu nilikuwa na laini NNE lakini mpaka sasa ni mbili tu ndio nazitumia yaani Tigo na Voda ingawa nilikuwa pia Airtel na Halotel.

Binafsi natumia zaidi Tigo lakini nikishafika uswahilini Kimara internet ni mpaka usiku SAA tano na kuendelea ndio napata. Kwa hiyo ndipo nilipoamua kuanza kutumia Voda. Voda kwa kweli wako vizuri sana ingawa tatizo gharama tu.

Kutokana na gharama za Voda kuwa juu sana nikawa na laini ya Airtel, lakini nao ugonjwa ni uleule kama Wa Tigo nikifika uswahilini tu yaani mpaka bundle la internet lina-expire. Hata Halotel licha ya kusifiwa sana lakini huko ninakokaa ni tatizo lilelile.

Nilichogundua ni kuwa kila mtandao una baadhi ya maeneo uko vizuri kulinganisha na mitandao mingine. Ila bado kwa ujumla Vodacom wako vizuri zaidi kulinganisha na wengine katika internet licha ya kuwa na subscribers wengi zaidi. Kwa waliosema kizuri hakikosi kasoro basi kasoro ya Vodacom ni bei tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…