Halotel janga jingine

Halotel janga jingine

Kiukweli natumia Halotel ila Speed yake imepungua Siku hizi haiwezi Kustream Live mpira ina goma goma sana
 
ila hii halotel nami imeanza kunisumbua siku za hivi karibuni... bado ipo vizuri ila speed yake imepungua kuna muda inasumbua sana... sua morogoro
 
Mimi mwenyewe sio naongea kwa kubahatisha nimetumia mitandao yote kwenye internet ila nilicho kuja kugundua halotel speed yao sio kubwa ila nikwamba inapatikana maeneo mengi hasa vijijini na inakuwa ni full 3G network ila sio kwamba ina speed kubwa watu wanadanganyika.,,nilikuja kuhakikisha hilo nilipokuja kukaa eneo ambalo mitandao yote inashika 3G network nikaja kupima speed ya internet aise Halotel anakimbizwa vibaya sana na Vodacom.
voda maeneo inapo patikana 3g nitamu pia
 
  • Thanks
Reactions: 7ve
ni kweli kwa baadhi ya maeneo halotel inazingua sana, sio speed ila inakatakata kuna inasoma kabisa 3g lakini hata page moja haifunguki.
Ukiikutia inashika vizuri aaaa utapenda mwenyewe.
Binafsi wamenihuzunisha tu baada ya kuambiwa tar 19 ile kuperuz youtube bure haitakuwepo tena... but all in all halotel is the best kwa ishu ya internet na speed
 
Halotel IPO vizuri sana labda simubyako kimeo mm napata H+muda mwingi ikishuka no 3G
1473870416706.png
1473870416706.png
 
Ukweli ni kwamba hawa jamaa limekuwa janga. Sio Songwe pekee, hata Mbeya ni tatizo. Mjini Mbeya ni mwendo wa kobe, na baadhi ya wilaya kama mbalali wengi wametupa simcard zao. Ukija hapa Iringa majanga. Hapa bongo maeneo ya kiwalani hakuna kitu ni mwendo wa kinyonga. Wacha turudi tulikotoka waendelee kutukamua lakini tupate Internet ya maana.
 
Wandugu baada ya kuujua huu mtandao hakika nilijua nimepata mkombozi ambaye atanifanya niwe kasi hasa kwenye issue zangu za mtandao. Hii ni wiki ya tano tangu halotel mahala nilipo imeanza kusumbua hakuna cha 3g iliyotulia.

Hili tatizo si kwangu tuu, karibia watu wangu wote wa karibu eneo nililopo wananiambia inazingua yaani bora hata kobe wangu voda ambaye nasikia huko mjini ana kasi ya ajabu.

Mwanzoni mwa mwezi huu niliamua kuwapigia watoa huduma nikaambia internet iko vizuri labda sehemu nilipo ndio kuna shida, nikaahidiwa kwa niaba ya wenzangu kuwa watashughulikia hadi leo kimya. Kinachoniuma zaidi nina bonge la bundle la mwezi sasa sielewi kama.

1. Walikuja na nguvu ya soda sasa wamezidiwa?

2. Kama ni tatizo la muda ndo liwe zaidi ya wiki 3?

3. Au wamekula kidogo kitu ili wapunguze ushindani ktk soko

Ni hayo tu.

Niko mkoa mpya wa Songwe wilaya ya Ileje.
Hata huku mjini ni shida tupu
 
Halotel ni kiboko yao haya majungu tu! Wengine wote wajipange! Dar mpaka tukuyu,manyoni mpaka kigoma!
Sio majungu kiongozi, hawa jamaa wamifanya nibadilishe simu nikiamini kuwa simu nitumiazo pengine zinamatatizo. Lakini baada ya kubadili nyingine ndipo nilipogundua kuwa Internet yao iko chini. Tena chini sana kiasi mambo mengine muhimu huwezi kufanya.
 
  • Thanks
Reactions: 7ve
Halotel ni bomba kama inazingua basi ni aitel yako mbovu
 
Halotel ni nafuu vifurushi vyake, ina kasi, huko ileje hata ikisumbua sio mbaya maana ni mbali sana usiwalaumu. Kama unabisha jaribu tigo au airtel.
 
Back
Top Bottom