Halo Quiz huduma inayokufanya kushinda zawadi nyingi kutoka halotel

HALOTEL VAS

JF-Expert Member
Apr 7, 2016
276
37
12809513_1712208439025907_6551092530102990359_n.png

UTANGULIZI

HALO QUIZ ni huduma inayowapa fursa watumiaji wa HALOTEL nafasi ya kushinda zawadi nyingi. Kwa kujibu idadi ya maswali kadhaa kwa usahihi kwa muda mchache.

JINSI YA KUTUMIA HUDUMA

Kujisajili

üMteja wa HALOTEL anaweza kujiunga na kuanza kutumia huduma hii nzuri kwa kupiga 0901221111.

üMtumiaji atapokea taarifa ya ujumbe wa kufanikiwa kusajili huduma na kupewa nafasi ya kucheza HALO QUIZ.

üKisha mtumiaji ana nafasi ya kuchagua kifurushi cha maswali na kuanza kujibu maswali.


Kusitisha huduma

üMtumiaji anaweza kujiondoa kwenye huduma kwa kupiga 0901221111.

üKisha chagua namba 9 kusitisha huduma.

üIkifuatiwa na namba 1 kuthibitisha usitishaji wa huduma.


Huduma ina vifurushi 4 vya maswali;

üKifurushi cha maswali matano: Maswali 5; Zawadi: Tsh. 2,000

üKifurushi cha maswali kumi: Maswali 10; Zawadi: Tsh. 4,000

üKifurushi cha maswali ishirini: Maswali 20; Zawadi: Tsh. 8,000

üKifurushi cha maswali thelathini: Maswali 30; Zawadi: Tsh. 16,000

FAIDA ZA HUDUMA:

üHuduma inampa mtumiaji wa HALOTEL ujuzi mpya katika nyanja mbalimbali, zikiwemo za

ü Sanaa, Sayansi, Hisabati,Mazingira , Historia, Michezo n.k

üHuduma hii, Inamwezesha mtumiaji wa HALOTEL kuweza kushinda hadi Tsh. 16,000.

GHARAMA ZA HUDUMA

üGharama za huduma ni Tsh.100 kwa siku.

üBaada ya kujiunga utapata nafasi mbili za kucheza HALO QUIZ bure.

üKisha mtumiaji atapaswa kulipia Tsh.100 kwa kila nafasi mbili za ziada kucheza HALO QUIZ.



VIGEZO NA MASHARTI


üHuduma hii ni kwa watumiaji wa HALOTEL pekee.

üHuduma ni kwa mteja wa malipo kabla na baada mwenye uwezo wa kupiga na kupokea.

üKwa kila kifurushi, mtumiaji atapata nafasi 2 za kucheza HALO QUIZ.

üMtumiaji anaruhusiwa kuchagua upya kifurushi chochote zaidi na zaidi.

üMtumiaji atatozwa gharama za kifurushi kila unapohitaji kifurushi upya.
 
Hii ya kujitoa mbona inakataa, acheni usanii mtu akijiunga kwa hiari mruhusu pia ajitoe kwa hiari.
 
Hii ya kujitoa mbona inakataa, acheni usanii mtu akijiunga kwa hiari mruhusu pia ajitoe kwa hiari.
Pia hawa jamaa wanavyofanya sio vizuri kwanini mnamuunganisha mtu kwenye huduma bila yeye kujiunga.. Alafu pia wanatoa maelezo ya kujitoa ya uongo. Pia ukipiga namba hiyo unazidi kuliwa pesa.. Mbaya zaidi hakuna customers care kweli mmesha nichafua TCRA liangalieni hili juu ya hawa halotel
 
Back
Top Bottom