Halmashauri zinakufa, Wabunge mko wapi

Halmashauri hizi zilikuwa na mchwa kweli kweli. Sasa baada ya dawa ya kuua hawa mchwa kupuliziwa kila mchwa anatafuta pa kutokea. Wengine wanakufa, wengine njaa kali maana chakula kina sumu. Mbaya zaidi, mpulizia dawa ndio kwanza anaanza!
 
Naona zile cheki zenu za lipa/pay Ded aka mkurugenzi mtendaji halafu mnaenda kugawana weekend zimeisha,Safi sana mlitumia vibaya kodi zetu,Si mishahara mnapata ,Hayo ndio mabadiliko ya kweli
 
Acha kulalamika fanya kazi.
Akili za ccm hizi. Utafanyaje kazi bila pesa?

Pesa hakuna, huko halmashauri wanalamika hakuna hata vifaa bado mnawaambia wafanye kazi.
KWANN NYINYI HAMKUSAINI MUSWAADA WA HABARI BILA MILION 10 KWA KILA MBUNGE?
KWANN PESA ZA WAHANGA WA TETEMEKO LA ARDHI MEZICHUKUA?
 
Wewe utakuwa miongoni mwa wezi waliokuwa wanaibia halmashauri. Mlizoea kuiba, kujiandikia madokezo hewa hata kazi hakuna, mlizoea kuandika madokezo yanayohusisha hata watu wa chini kama wahudumu na mwisho wa siku hamuwapi hela mnaliza wenyewe, mlizoea kuwaandika baadhi ya wafanyakazi kuwa mmefanya nao kazi na mwisho wa siku mnawanyima hela, mlizoea kuandika eti kazi fulani imefanyika kwa milioni kadhaa kumbe hata kazi hakuna, mlizoea eti kupeleka ripoti mkoani (unaweza kukuta ni umbali wa kutoka kariakoo kwenda mnazi mmoja) mtu anadai alipwe milioni moja na zaidi. Mimi kuna watu wanafanya kazi halmashauri wala hakuna kitu kama ukata kwao ila wanawashangaa tu wanaolalamika hasa wale wezi kama mleta maada. Mkome kabisa Dkt Magufuli usilegeze kabisa baaanaaaaaa hao wezi wa halmashauri. Na ningefurahi kama wangewapunguza kabisa nyie wezi wezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…