Halmashauri zetu na mapungufu yake.

Saitot

JF-Expert Member
Apr 3, 2013
613
151
habari zenu wana jamvi,
Nikiwa kama mtumishi wa serikali nimebahatika kufanya kazi Halmashauri za miji/jiji na watu mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya Tanzania lkn niliyoyasikia na kuyaona yanasikitisha.
Halmashauri hizi ndizo zenye wafanyakazi wengi wakiwemo manesi, walimu matabibu na wafanyakazi wanaoitwa vibarua. Huku ndiko ambapo Makatibu wanashindwa kuwahudumia watumishi wao na maafisa Utumishi wanashindwa kutekeleza wajibu wao wakiwa kama viongozi ,na unaishia kutokujua nani mkubwa kati ya hawa wawili, kwa mfano :kuna watumishi wamepandishwa vyeo muda mrefu lkn hawajawahi badilishiwa mishahara yao kwa kipindi mpaka cha miaka mitatu,yaani cheo chako kinakutana na cheo kingine???huku ndiko wahasibu wanakula hela za malipo ya wafanyakazi bila woga na kukusainisha lundo la makaratasi tofauti na kiwango ulicholipwa.
lkn jambo linalotia mashaka zaidi hawa hawa viongozi wetu wanaishia kusema halmashauri zote zipo hivi hivi ,yaani matendo yao yanafanana, sitaki kuamini hili yaani halmashauri ya jiji Tanga wafanye kama harmashauri ya jiji Mbeya?
Mwisho naiomba serikali kumulika hizi harmashauri zote ili muweze kuyaona haya niliyoyasema wafanyakazi wanateseka sana wamekuwa watumwa wa maafisa utumishi na makatibu .
 
Back
Top Bottom