Halmashauri za CHADEMA zaongoza kwa usafi.

Halmashauri za CHADEMA zaongoza kwa usafi.

Chadema yenyewe safi,ila kwa Arusha mhh!!hapo umeniacha mbali,labda kama ni usafi wa mwili na mavazi,ila kwa mazingira arusha ni CHAFU balaa,ukiondoa barabara inayotokea moshi maeneo ya phillips hadi mianzini ndio yenye unafuu,katikati ya mji hapafai.

mkuu olyset,
city council ya arusha inaongozwa na chama gani?
 
Pamoja sana kamanda!
Ilitolewa fungu kwa ajili ya usafi wa mazingira, akina Lyimo sijui wameenda kujengea mabaa oloirieni!

kabisa kule chini kila baada ya nyumba bar mpaka moshono
 
Niko mwanza,jamani kwa hapa mwanza wamejitahidi bwana!
Barabara safi,sokoni kuko poa kabisa,mahospitalini,vyoo vya town safi aah mwanza nawapa Big up!
Kweli likizo ikifika huwa najifikiria kurudi dar mara2*2:
 
Roho ikiwa safi na mwili utakuwa safi.Huwezi kuwa na roho safi ukawa na mwili mchafu,ila unaweza kuwa na mwili safi ukawa na roho chafu.M4C DAIMA
 
Hata Manispaa ya moshi wanaopigwa faini ya kuchafua kama kukojoa kwenye kuta , kutupa takataka, kutema mate kwasababu ya kula kuberi na Ugoro na kujisaidia haja kubwa ni wanachama wa CCM
 
vp Karatu, Iringa mjin, Mbeya mjini, mbozi magharibi, ubungo, kawe, hai, singida mashariki, kwa zitto...mbona wao hawajitahidi

Unaelewe nini juu ya kuongoza halmashauri za mji/jiji? Hayo ni majimbo yanayoongozwa na chadema lakini madiwan wengi katika hayo majimbo wanatoka ccm, hao ndio wanao-unda halmashauri si mbunge mmoja.
 
Unaelewe nini juu ya kuongoza halmashauri za mji/jiji? Hayo ni majimbo yanayoongozwa na chadema lakini madiwan wengi katika hayo majimbo wanatoka ccm, hao ndio wanao-unda halmashauri si mbunge mmoja.
karatu ipo chini ya cdm yote...tarime ipo chini ya cdm yote, songea mjini pia chini ya cdm yote..hakuna usafi. pia mimi cjaongea kwa maana ya kupinga, na challenge tu hizo kwa halmashauri husika
 
Kazeni buti makamanda ila wekeni angalizo 2015 kwani 2010 kuna baadhi ya makamanda wamekosa ubunifu na kupwaya katika ngazi za udiwani huenda ni ugeni au wamesahau hoja za kuzisimamia.

DO IT HARDER 2015
 
wacheni ushabiki, usafi gani mnauzungumzia? umefika dambo wewe pale uhuru? umeiona unguja? umeenda rwagasore yote, soko kuu na kule national? usafi wanaouzungumzia ni kwa kulinganisha na mji mkubwa kama dar. sasa mwanza yenye mitaa miwili, itaonekana kuwa safi kwa dar coz wao wana mitaa 20. lakini si kusema kuwa mwanzan ni safi kivile
 
huwezi ukatulinganisha na hao nagamba hata siku moja.....gwanda ni alama ya usafi.
 
Nimefurahi sana kusikia Halmashauri 3 ambazo ni ngome ya CHADEMA zimeshika nafasi 3 bora katika usafi wa miji na majiji.

Hii inamaanisha, tukitaka miji safi, basi Halmashauri zote ziongozwe na CHADEMA.

1. Mwanza
2. Moshi
3. Arusha

Chanzo: Taarifa ya Habari ya Channel Ten ya saa 1 usiku, tarehe 5 Juni 2012.

Hongera mwanza kwakuweza kumshusha mosh at the top alikokaa siku nyingi nadhani sasa ushindani utakuwepo na usafi utapewa kipaombele ktk halmashauri zetu
 
Hiyo inatokana na Chadema kupata kura nyingi kwa wasomi, sasa nyinyiem wanapata kura kwa wajinga na maskini wakutupa usafi watafanya sa ngapi, watz tubadilike

acha kutukana watz wewe,tuheshimiane,matusi ya nini?mjinga ni nani? Ni wewe mwenyewe unayeweka ujinga wako humu jf,shinyanga walioichagua chadema kuliko mkoa wowote tz ni wajinga?kisa hawajapata hati ya usafi? Jf inatakiwa kuwa makin sana,badala ya kujenga mtazidi kubomoa na kuleta uchonganishi mkubwa kati ya jamii moja na nyingine,angalien sana.
 
Back
Top Bottom