Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma inatangaza nafasi 8 za kazi

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
1,587
2,000
KUMBU. NA. KSDC/S.2/19VOLII/21
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu anayo furaha kuwatangazia watanzania wenye sifa za kuomba nafasi za kazi zifuatazo:

MTENDAJI WA KIJIJI III NAFASI 3

Sifa za jumla
Mwenye elimu ya kidao cha IV au VI aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo Utawala , Sheria, Elimu ya jamii usimamizi wa fedha maendeleo ya jamii na sayansi ya jamii kutoka chuo cha Serikali za mitaa Homboro Dodoma au chochote kinachotamblika na serikali

KAZI NA MAJUKUMU
 • Afisa mshauri na mtendaji mkuu wa Serikali ya Kijiji
 • Kusimamia ulinzi wa raia na mali zao kuwa mlinzi wa manai na msimamizi wa utawala bora
 • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipnago ya maendeleo ya kijiji
 • Kutafsiri na kusimamia sera, sheria na taratibu
 • Kuandaa taaarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na na kuongeza uzalishaji mali
 • Kiongozi mkuu wa vitengo vya kitaalamu katika kijiji
 • Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu waliopo katika kijiji nk
 • Kupokea kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi
 • Atawajibika kwa mtendaji wa Kata
MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi ya mishahara ya serikali yaani TGS B Kwa mwezi


NAFASI: KATIBU MAHSUSI (Nafasi 1)

Sifa za Ujumla
Mwenye cheti cha mtihani ya kidato cha IV, aliyehudhuria mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya tatu, awe amefaulu somo la Hati mkato ya Kiswahili na kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na awe amepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Selikali na kupata cheti katika program za windows, Microsoft Office, Internent, E-mail na Publisher

KAZI NA MAJUKUMU
 • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida
 • Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa
 • Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni tarehe za kutekelezwakatika ofisi anamofanyia kazi na kumuarifu mkuu wake kwa wakati unaohitajika
 • Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake wa majadala, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini
 • Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msismamizi wake wa kazi

MSHAHARA: Ngazi ya mshahara TGS – B

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II NAFASI 4

SIFA ZA KUAJIRIWA
Kuajiriwa wahitimu wa kidfato cha 4 na 6 wenye cheti cha utunzaji wa kumbukumbu katika mojawapo ya fani zifuatazo, Afya, Masijala, Mahakama na Ardhi

KAZI NA MAJUKUMU
 • Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaiili yanayohitajiwa na wasomaji
 • Kudhibiti upokeaji uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka
 • Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu katika makundi kulingana na somo husika
 • Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki katika masijala/vyumba vya kuhifadhi kumbukumbu
 • Kuweka kumbukumbu katika mafaili
 • Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kuotka taasisi za serikali
MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi ya mishahara ya serikali yaani TGS B Kwa mwezi

MASHARTI YA JUMLA
 • Waombaji wawe ni raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
 • Barua za maombi ziandikwe kwa mkono na mwombaji mwenyewe na zitumwe kwa njia ya posta tu
 • Mwombaji anatakiwa kuambatanisha nakala za vyeti vya elimu na vyeti vya taaluma cheti cha kuzaliwa na wasifu wenye mawasiliano sahihi ya simu
 • Transcripts, testimonials hazitakubaliwa

Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA,
S.LP. 97
KASULU.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 25 February, 2019.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom