Halmashauri ya Mwanza ni ya Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Halmashauri ya Mwanza ni ya Chadema

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kilimasera, Nov 4, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) jijini Mwanza kimeshinda jumla ya kata 11 kwa nafasi ya udiwani kati ya kata 19 zilizoshiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

  Kwa upande wa CCM kimeweza kupata ushindi katika kata nane kwa majimbo ya Ilemela na
  Nyamagana.

  Kwenye uchaguzi huo Chadema ilipata ushindi katika majimbo ya Nyamagana na Ilemela kwa kata zilizokuwa zinashikiliwa na CCM.

  Kwa upande wa Chadema katika jimbo la Ilemela kilipata ushindi wa katika Kata za Kirumba ambapo diwani wake ni Novatus Manoko, Kata ya Kitangiri (Henry Matata), Kata ya Nyakato (Manyerere), Kata ya Pasiansi(Rose Brown), Kata ya Ilemela (Marietha Chenyenge), na Abubakari Kapela aliibuka mshindi katika Kata ya Nyamanoro.

  Kwa upande wa jimbo la Nyamagana, Chadema kilishinda nafasi ya udiwani kwa kata tano. Kata hizo na madiwani wake kwenye mabano ni Kata ya Igoma( Adam Chagulani), Kata ya Mahina (Chalres Chichibera), Kata ya Pamba(Samwel Range), Kata ya Mbugani (Hashim Kijuu) na Kata ya Isamilo diwani aliyechaguliwa ni Pius Boniphace.

  Kwa upande wa CCM, kilipata ushindi katika kata nne zifuatazo na madiwani wake kwenye mabano, kata hizo ni Kata ya Mkolani(Stanslaus Mabura), Kata ya Buhongwa (Reuben Nzari) na katika Kata ya Igogo John Minja ambaye alifanikiwa kutetea nafasi yake ya udiwani, Kata ya Butimba Dismas Masunu naye aliitetea nafasi yake ya udiwani kwa kuibuka mshindi na katika Kata ya Nyamagana Bhiko Kotecha naye aliitetea nafasi yake ya udiwani kwa kuibuka ushindi.

  Katika jimbo la Ilemela CCM iliibuka mshindi kwa kupata viti vitatu vya udiwani katika kata za Bugogwa, Sangabuye na katika Kata ya Buswelu.

  Hata hivyo wakati kata hizo 19 zikihitimisha mbio za uchaguzi na kufanikiwa kuwapata wawakilishi wake, Kata za Mkuyuni na Mirongo zilizoko katika jimbo la Nyamagana hazikushiriki kwenye zoezi la uchaguzi kutokana na kile kilichoelezwa na Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza, Wilson Kabwe kuwa kulikuwa na upungufu wa baadhi ya vifaa muhimu vya kupigia kura.
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Matokeo ya sehemu nyingine kwa kiasi fulani yataathiri maamuzi ya wapiga kura wa hizi kata
   
Loading...