Halmashauri ya arusha yavunja mkataba wa kifisadi kwa shinikizo la diwani wa chadema

Mwan mpambanaji

JF-Expert Member
Apr 3, 2008
482
131
Leo halmashuri imevunja mkataba wa kukusanya ushuru katika soko la kilombero, kati yake na kampuni ya piga deal, ni baada ya malumbano na shinikizo kubwa kutoka kwa diwani wa kata ya levolosi kwa tiketi ya chadema Mh Nanyaro, kampuni hii imeshindwa kukusanya ushuru na inadaiwa mamilion ya fedhwa na halmashauri.

Jana kulitokea malumbano makali kati ya huyu diwani akiungwa mkono na wafanyabiashara, mkurugenzi wa manispaa pamoja na mkurugenzi wa hii kampuni inayodaiwa kuwa ya watoto wa kigogo mmoja.
 
Big up nanyaro diwani mwenye umri mdogo kuliko wote kwenye halmashauri lakini unachapa kazi kuliko baba na babu zako mnaofanya nao kazi
 
wanaarusha jf wanasemaje juu ya mkataba huo, je ni wa kifisadi?? kama ni hivyo-big up mhe. diwani. wembe ni ule ule kuondoa mafisadi
 
Kamanda Nanyaro safari ya kwenda kugombea Ubunge Arumeru hiyo!NAKUKUBALI SANA NANYARO MKUU,Wewe siyo Mnafiki,siyo Mbabahishaji,siyo Mmumunya maneno unafuata nyayo za Rais W.P.Slaa rais wetu wa Moyoni.
 
Makamanda nawashukuru sana,
ni kweli kuwa mkataba umevunjwa rasmi leo, baada ya wakala kushindwa kutekeleza majukumu yake, na mkataba ulikuwa na utata, kesho ntatoa maelezo vizuri baada ya mkutano wangu na wananchi asubuhi
 
Giddy Mangi,sifanyi ili niwe mbunge nafanya kwa ajili ya wananchi,na ni wajibu wangu kuwatetea wasiokuwa na sauti,
 
nanyaro, nimependa msimamo wako juu ya mikataba ya kifisadi, natambua wafanya hv kwa mapenzi ya wananchi wako, zaidi nimependa ulivyojitokeza JF na kuongea na makamanda!

Mungu akuongoze, akujaze ujasiri na akuondolee uwoga ktk mapambano. Tupo nyuma yenu Makamanda wengi tu, tutapambana mpaka mwisho!
 
Makamanda nawashukuru sana,
ni kweli kuwa mkataba umevunjwa rasmi leo,baada ya wakala kushindwa kutekeleza majukumu yake,na mkataba ulikuwa na utata,kesho ntatoa maelezo vizuri baada ya mkutano wangu na wananchi asubuhi

Nanyaro tunakuamini utaleta mapinduzi makubwa katika jiji letu la Arusha, kazi ile ile ya kuwasaka na kuwatokomeza mafisadi ktk jiji letu na nchi nzima!!!!!!
 
Makamanda nawashukuru sana,
ni kweli kuwa mkataba umevunjwa rasmi leo,baada ya wakala kushindwa kutekeleza majukumu yake,na mkataba ulikuwa na utata,kesho ntatoa maelezo vizuri baada ya mkutano wangu na wananchi asubuhi
kazi nzuri kamanda hicho ndio tunachotarajia kutoka kwenu na ndio tunapoweka tofauti na hawa mafisadi kiutendaji.........
 
Keep it Up Nanyaro, endelea kuwatetea wananchi, sisi wana arusha tuko nyuma yako mkuu! aluta continue!
 
Colleagues,

Halmshauri nyingi nchini zinamatatizo kama hayo. Wananchi wangejua kuwa mbinu yakuwa na Mawadiwani wengi wa CCM ni kuendeleza uvundo wa rushwa wangeliamka na kuchagua mawadiwani vyama vingine.

I really I appreciate the hard work of CHADEMA in Arusha. You are making Arusha a model of CHANGE for other halmashauri in the country.
 
Back
Top Bottom