Chakaza
Platinum Member
- Mar 10, 2007
- 41,031
- 74,722
Rais mahali popote ni alama ya taifa na ndio maana hata kama yapo mambo watu hawamuungi mkono bado hawawezi kukubali heshima ya taasisi yake ikashuka huko nje ya nchi kwani kwa kutokea hilo ni nchi nzima imefedheheka.
Makonda amejenga tabia ya kutaka kumpa sifa hata za uongo Rais Magufuli kiasi cha kufikia kumfedhehesha mbele ya jamii.
Mfano wa karibu ni ujio wa meli ya matibabu ya China inayozunguka duniani kutoa tiba ya BURE.
Makonda ameibuka na kusema Magufuli kalipa gharama kuwezesha meli hiyo kuja kutoa tiba kwa vile anawapenda sana watu wake. Huu ni uongo wa wazi, na kwa vile haujakanushwa na Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu (pengine kwa kumuogopa mtoto mpendwa) basi wajuaji wanadhani katumwa na JPM mwenyewe kutamka hayo.
Nje ya nchi tunaonekana mazoba kwa kulishwa upupu huo na hata hao watoa msaada wanatuona sisi na Rais wetu ni wa ajabu sana.
Serikalini chini ya PM na waziri wa TAMISEMI wameonyesha kumgwaya huyu jamaa, jee Halmashauri kuu ya CCM inayokutana sasa hivi haiwezi kuondoa aibu hii kwa Mwenyekiti wenu na Rais wa jamhuri?