Halima Nassoro kada CCM anayepora viwanja, kumg'oa Masanja Mwanza

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Halima Nassoro kada CCM anayepora viwanja, kumg'oa Masanja Mwanza

Miezi minne sasa tangu sakata la uuzwaji wa viwanja viwili katika eneo la Rwagasore jijini Mwanza kuibuka, mapya yaibuka.

Viwanja vilivyouzwa ni viwanja namba 191 hadi 1996 ambavyo viliuzwa kinyemela bila kufuata taratibu za manunuzi.

Moja ya mambo yaliyoibuka ni kuhusu aliyekuwa Afisa ardhi wa Jiji Halima Nassoro, aliyehusika kuchora mchongo wa kuuza viwanja hivyo kwa shilingi bilioni 1 lakini uhalisi wa mauzo ya viwanja hivyo ni zaidi ya shilingi bilioni 3.

Sakata lililoibuka kwa sasa ni kuhusu Halima, kutapeliwa na kigogo mmoja jijini Mwanza kiasi cha Shilingi milioni 300 kama mgao wa uuzaji wa viwanja hivyo.

Katika uuzaji wa viwanja hivyo, Halima ndiye alienda kuchukua fedha hizo kutoka kwa kigogo mmoja katika wizara ya ardhi.

Baada ya kuchukua fedha hizo taslim, alizifikisha kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Mwanza na kuanza kupanga utaratibu wa kuwanyamazisha baadhi ya viongozi wakiwemo wa chama cha Mapinduzi.

Miongoni mwa watu walioonjeshwa asali ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji, Sekiete Yahya, Mwenyekiti wa kamati ya mipango miji (Milioni 150 za kuwagawia madiwani wenzake)

Mchezo upo hivi, baada ya Halima kuchukua mgao wake huo alienda kuweka katika akaunti ya kigogo huyo ambaye kwa sasa amegoma kurudisha na kukana Halima kumpa kiasi hicho cha fedha. (akaunti no ya kigogo huyo inahifadhiwa).

Halima alichukua kiasi hicho cha fedha na kuweka katika akaunti ya kigogo huyo ili kukwepa uchunguzi uliofanyika usibaini kama anaweza kuwa na fedha hata hivyo bado uchunguzi umebaini amehusika na uuzwaji wa viwanja hivyo.

Kufuatia mgogoro huo wa Halima na kigogo huyo kwa sasa ni maadui wakubwa na imefikia hatua ya kutoleana lugha za vitisho.

Pamoja na hilo, Taarifa za ndani zinaeleza kuwa Halima na vigogo wengine wa Jiji la Mwanza wameuza kiwanja cha wazi kilichopo eneo la Uhuru kwa gharama ya shilingi bilioni 1.

Kiwanja hicho kipo jirani na bar maarufu jijini Mwanza ya Frolida ambako sasa kiwanja hicho kimejengwa mgahawa.

Mtu anayetajwa tena kuhusika na uuzwaji wa kiwanja hicho ni Halima Nassoro, ambaye ndiye anafanya mipango yote ya upigaji kwa ushirikiano na aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji hilo.

Inaelezwa Halima ambaye ni kada wa chama tawala cha CCM, wizi huo anaoufanya anajiandaa kugombea ubunge wa viti maalumu.

Halima anachota fedha hizo na kuzificha akilenga kumg'oa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Marry Masanja ambaye ni Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mwanza.

Fedha anazoiba inatajwa atazitumia kuwahonga wajumbe kama alivyofanya katika uchaguzi wa ndani wa chama cha Mapinduzi CCM na kupata nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa kutokea wilaya ya Nyamagana.

Kwa mjibu wa Mwandishi wetu, inaelezwa Halima alipotafutwa kwa njia ya simu, alikana kuhusika na uuzwaji wa viwanja hivyo na kwamba uuzwaji ulifuta taratibu zote.

Soma hapa chini

Kati ya januari 25- 26 mwaka huu mkuu wa mkoa alitoa taarifa kuhusu wizi huo na hapa chini ndiyo ilikuwa kauli yake.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima 'amemshtaki' mkurugenzi wa jiji hilo, Selemani Sekiete kwa Wizara ya Tamisemi ambayo ndio mamlaka yake ya nidhamu, akimtuhumu kuhusika na uuzaji wa viwanja viwili vyenye thamani ya Sh1 bilioni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo Ijumaa Januari 13, 2023, Malima amewataja wanaosimamishwa kazi kwa nyadhifa zao kuwa ni mhasibu wa Jiji, mwanasheria, ofisa manunuzi na ofisa mipango.

Watumishi hao wa umma wanadaiwa kuuza viwanja hivyo vilivyopo mtaa wa kibiashara katikati ya jiji kwa thamani ndogo kulinganisha na bei ya soko.

Amesema walishirikiana kuuza viwanja hivyo bila kufuata utaratibu kinyume cha taratibu na maadili ya viongozi huku mkurugenzi wa jiji akidaiwa kukiuka maagizo ya kamati ya ulinzi Wilaya ya Nyamagana na ofisi ya mkuu wa mkoa.

"Kwa mamlaka yangu nimeelekeza ofisi ya katibu tawala Mkoa wa Mwanza iwasimamishe kazi watumishi wanne ambao ni wakuu wa idara kupisha uchunguzi na tunaandika barua ofisi ya Rais (Tamisemi) kwa hatua kuhusu mkurugenzi wa Jiji," amesema Malima.

Mkuu huyo wa mkoa amesema licha ya suala la maamuzi kuachwa mikononi mwa Tamisemi, mamlaka ya mkoa unaona kuwa kiongozi huyo amekosa sifa za kuendelea kusalia mkoani humo.

Ameagiza idara ya ardhi kuangaliwa upya pamoja na watumishi hao wanne kuchunguzwa endapo wamehusika katika tukio hilo.

Maazimio ya kikao cha Ulinzi na Usalama wilaya ya Nyamagana Septemba 28, 2022 ilikataza kurejesha au kufanya uwekezaji wowote wa viwanja vitano kuanzia namba 191 hadi 196 bila kamati hiyo kufahamishwa.

Mwisho
 
Wakati mwingine akipata hela za dili lingine, azilete kwangu mara moja. Nitamtunzia kwa uaminifu mkubwa! Na mwisho wa siku tutagawana pasu kwa pasu.
 
Kwanini Halima unamtaja !
Sekiete unamtaja pia!

Lakini huyo kigogo hutaki kumtaja?

Nini kipo nyuma yako?
 
Wee Ni chawa wa naibu waziri acheni kumchafua afisa aridh bila sababu zozote kma anajipanga kugombea muacheni apambne siyo kumchafua kuwa ameiba viwanja vya watu ili kumuaribia taswira yake mbele ya jamaa
Halima kanyaga twende mam siasa Ni Vita na maisha vile vile ni vitaa
 
Mm nimefanya Kaz idara ya aridh nafaamu sna hujuma zilizoko kweny idara hyo

Ni idara yenye fedha nyingi sna hvyo imeleta wivu na husda kwa maafisa aridh

Arusha kila siku Ni mwendo wa mahakamani na maafda ardh
 
Nguchiro wanakaa kwenye shimo, ukitaka watoke, ni wabishi, wewe mwaga maji tu, hewa itaisha, wataanza kutoka.
 
Halima Nasoro siyo yule mwanamama aliesimamishwa kazi na Mh.Lukuvi enzi zile?
 
CCM tukishazungukana kwenye migao basi kinachobakia ni kuumbuana.

Wote ni wezi.

Tuiweke CCM pembeni

CC: ChoiceVariable
CCM wanagawa viwanja tangu lini?

Nilikuwa sijui kama Catres Rwegasira Yuko hapo, jamaa kanyooka sana, hana konakona, ngoja tuone mkakati wake, ili afanye kazi vizuri, wakubali wamuondolee watu wenye skendo, aanze na timu yake mpya.

Cha msingi aende na kiroba Cha majini na ndumba, hiyo Ofisi Ina walozi balaa
 
Back
Top Bottom