Halima Mdee Unachemka

Halima Mdee Unachemka

Yeye anajua ipo kwa mamlaka ipi ndio maana alikuja mwaka Jana na akahaidi kurudi kwetu ndani ya mwezi na solution ya tatizo letu, but ndio ikawa kimojaa, tunamuona kwa Luninga tu mjengoni.

hebu niambie serikali hii ya cc hemu imeanza lini kusikiliza sauti ya wananchi?.
 
sawa naomba uniambie hao majukumu yake kwa uchache,je na kama akafuatilia na kupuuzwa na wahusika ana mamlaka ipi kisheria dhidi yao?.
wakimpuuza anatakiwa kuja kutupa feedback wananchi kuwa swala lenu nimelipeleka na nimepuuzwa, then tunajipanga nae kufanya Maandamano ya amani kwenda mahala husika waliko mpuuza mbunge wetu. Haoni Lema mwezie kule Arusha au Sugu Mbeya? Haya yote yanakuja baada ya yeye kuja na kutoa ahadi na kusema atarudi ndani ya mwezi na hajarudi tena na hakuna taarifa yoyote kama amepuuzwa au lah? Wewe Baba yako akikuambia atakulipia Ada alafu unamuona amekaa kimya tu na siku zinaenda shule inakupita tu hautauliza?
 
hebu niambie serikali hii ya cc hemu imeanza lini kusikiliza sauti ya wananchi?.
Ndio tunatakiwa wafundisha kusikia sauti zetu via Wabunge, sasa kama wabunge ni mabubu unategemea hao cc hemu watasikilizaje? Kama hawasikiii unatakiwa kuwa na solution sio kukaa kimya tu, tulipoona chama kimoja kina legalega ndio tukaleta vyama vingi na tulipo ona katiba haitufai ndio tumeanza mchakato wa katiba mpya. umeona hapo ni shida na solution sasa wewe ukusema hawasikii then what? Mbunge ambae ni sauti ya wananchi anatakiwa kuwa LOUDER mnooo then watamsikia na kama hawasikii tunaandamana.
 
Watanzania wana tabu sana mkuu.

Wanataka Mdee akawajengee barabara.....Ukenge mwingine tabu tupu.

Mdee hana fedha hana serikali, anacho fanya nikuikumbusha serikali wajibu wake kutekeleza huduma za jamii ndicho anacho kifanya watu wanataka Mdee atoe fedha zake mfukoni ajenge barabara.
 
Mdee ni Sauti ya wananchi kwa serikali, Sisi hatujawahi mchagua mkurugenzi wa Jiji wa Meya wa Jiji. Eleweni majukumu ya Mbunge.

Sijasikia HATA SIKU MOJA, Halima kaamsha valangati Jijini au serikali hasa wizara ya ujenzi, ili barabara za Kawe zishughulikiwe.
Yeye ni kiguu na njia na M4C, waliomchagua wamelala solemba.

Tusirudie kosa hili come 2015
 
Jamani mleta uzi anania njema tu kwa Mdee lakini kwa kuwa Chadema huwa wanatabia ya kudharau ushauri wa wananchi hasa wasio na majina makubwa watapuuzia. Inaweza mgharimu hii Harima japo ni miongoni mwa wabunge wa chadema ambao nawakubali kwa kuchangia hoja zenye mtazamo wa kitaifa zaidi. Mdee anajiamini na hoja zake nyingi bungeni huwa zina mashiko, asichezee kazi achezee mshahara na posho asije jilaumu kwa kupokonywa jimbo au likarudi Jembe na nyundo mwaka 2015.
 
Mdee hana fedha hana serikali, anacho fanya nikuikumbusha serikali wajibu wake kutekeleza huduma za jamii ndicho anacho kifanya watu wanataka Mdee atoe fedha zake mfukoni ajenge barabara.
Sawa sasa hizo huduma zipo wapi mkuu? barabara nafikiri ni huduma ya jamii,alikuja aka ahidi atarudi now ni mwaka mzima hajarudi na kauna feedback. Mdee hana hela ya kusema tumuombe atujengee barabara umeelewa vibaya mkuu pole.
 
Jamani mleta uzi anania njema tu kwa Mdee lakini kwa kuwa Chadema huwa wanatabia ya kudharau ushauri wa wananchi hasa wasio na majina makubwa watapuuzia. Inaweza mgharimu hii Harima japo ni miongoni mwa wabunge wa chadema ambao nawakubali kwa kuchangia hoja zenye mtazamo wa kitaifa zaidi. Mdee anajiamini na hoja zake nyingi bungeni huwa zina mashiko, asichezee kazi achezee mshahara na posho asije jilaumu kwa kupokonywa jimbo au likarudi Jembe na nyundo mwaka 2015.
Wewe umenielewa kabisaa, mimi Point yangu ni kumuweka sawa na awe anakumbuka majukumu yake. Sisi ndio tupo ground zero inatupa ugumu sana kutetea hoja za CDM huku kama mambo yanakuwa hivi.
 
wakimpuuza anatakiwa kuja kutupa feedback wananchi kuwa swala lenu nimelipeleka na nimepuuzwa, then tunajipanga nae kufanya Maandamano ya amani kwenda mahala husika waliko mpuuza mbunge wetu. Haoni Lema mwezie kule Arusha au Sugu Mbeya? Haya yote yanakuja baada ya yeye kuja na kutoa ahadi na kusema atarudi ndani ya mwezi na hajarudi tena na hakuna taarifa yoyote kama amepuuzwa au lah? Wewe Baba yako akikuambia atakulipia Ada alafu unamuona amekaa kimya tu na siku zinaenda shule inakupita tu hautauliza?

ni kweli nitauliza,ok lema na sugu kwa upande wa cc hemu wametengenezewa picha ya ukorofi nashukuru angalau ww umeweza kuona kuwa huwa hawafanyi fujo.ila tz maandamano huwa ya amani pale inapotokea suala la kupongezwa serikali.naomba nikutoe nje ya mada kidogo hv madaktari waliwahi fanya fujo ktk historia ya nchi hii?.
 
Ndio tunatakiwa wafundisha kusikia sauti zetu via Wabunge, sasa kama wabunge ni mabubu unategemea hao cc hemu watasikilizaje? Kama hawasikiii unatakiwa kuwa na solution sio kukaa kimya tu, tulipoona chama kimoja kina legalega ndio tukaleta vyama vingi na tulipo ona katiba haitufai ndio tumeanza mchakato wa katiba mpya. umeona hapo ni shida na solution sasa wewe ukusema hawasikii then what? Mbunge ambae ni sauti ya wananchi anatakiwa kuwa LOUDER mnooo then watamsikia na kama hawasikii tunaandamana.

unaonaje wananchi nchi nzima wakianza kuandamana kwa ahadi za je kei ambazo hazikutekelezwa?.
 
Yes ndivyo inavyotakiwa na ndio demokrasia! kama huwajibiki unatolewa tu madarakani,maana wakati una ahidi uliona vinawezekana baada ya hapo unakuwa bize na mabo mengine,ndio alicho kifanya mh. Mdee kwetu mwaka mmoja uliopita. and sio style yetu kabisa wana CDM ya kutotimiza ahadi. Mambo ya longolongo ni huko kwa akina JK.
 
ok ww binafsi ulishawasiliana na mdee kama mbunge wako na mwanachama mwenzako na kufahamu tatizo lipo wapi? na kama hapana kwanini,je muda wote huo hajawahi fanya mkutano na wapiga kura wake?,au hata wa chama ambako naamin wewe kama mwanachadema unpepata nafasi ya kuhoji kile kinachokukera.
 
Baada ya ule mwezi kupita amekumbushwa mnoo na viongozi watendaji wake na majibu tunayopata nikuwa yupo bize,nikipata muda ntaenda omba nakala za barua alizoandikiwa na hajajibu hata mmoja zaidi ya kupiga simu tu kwa viongozi wetu. mimi ningekuwa na simu yake, email yake etc ningekuwa nimefanya effort zangu na kampeni zangu kama hizi kuleta attention na kumbusha majukumu yake. Kwa ufupi ametutupa na hasemi lolote sasa sijui sisi huku ndio sio sehemu ya jukumu lake au lah? kama una email yake au simu yake nipatie I will do the rest.
 
Mdee anakusanya kodi Kawe?

Yeye anatakiwa apige kelele huko serikalini ili wananchi wake wapatiwe huduma. Ukipiga kelele angalau utapata pesa ya miradi miwili mitatu. Ukikaa kimya ndio kwanza hela zitaenda majimbo ya ccm. Ila mashuleni naona kajitahidi madawati na komputa keshatoa.
 
Naona mmeshatumwa na mke wa slaa ili kumnyang'anya mdee jimbo ili apate yeye.Kweli cdm ni SACCOS, mbona mnasema wabunge wa cdm wanafaa sana?inakuwaje sasa?Huu mpango mdee ameshaushitukia ndio maana ameamua sasa kuungana na ZITTO ili awaumbue zaidi.Jamani SACCOS hii(cdm) ndo inakufa hivyo wenye hisa wakachukue chao.
 
Sawa sasa hizo huduma zipo wapi mkuu? barabara nafikiri ni huduma ya jamii,alikuja aka ahidi atarudi now ni mwaka mzima hajarudi na kauna feedback. Mdee hana hela ya kusema tumuombe atujengee barabara umeelewa vibaya mkuu pole.

Sigara zile anazoendekeza zinampa mzuka wa m4c na zinamsahaulisha mambo ya jimboni kwake
 
Back
Top Bottom