Halima Mdee: Sirro hana mamlaka ya kuzuia kumjadili Lissu, na Shehe Ponda kafanya Uchochezi gani?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Mbunge wa Kawe kupitia CHADEMA, Halima James Mdee, amejibu kauli ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Nyakoro Sirro ya kutojadili suala la Tundu Lissu, na kusema hawatoacha kufanya hivyo.

SIRRO.jpg

Kwenye ukurasa wake wa twitter Halima Mdee ameandika ujumbe akisema kwamba hakuna sheria inayokataza mtu kujadili jambo fulani, na IGP hana mamlaka ya kukataza hilo.

“Hakuna popote katika sheria za nchi IGP ana mamlaka ya kunyamazisha watu wasijadili jambo, tutaendelea kujadili ya Lissu mpaka haki itendeke”, ameandika Halima Mdee.

Pia Halima Mdee ameendelea kwa kuandika kuhusu kukamatwa Sheikh Ponda, akisema ni mipango ya kuwafunga mdomo watu watakaojadili suala hilo.

“Najaribu kutafakari alichokisema Ponda na kwa namna gani kinaashiria uchochezi, sikioni! ni namna ya kutisha na kufunga midomo watu”, ameandika Halima Mdee.

Hivi karibuni IGP Sirro aliwataka wanasiasa kuacha kufanya mijadala ya kumjadili Tundu Lissu, na waliache jeshi la polisi lifanye kazi zake bila kuingiliwa na jana Jeshi la polisi lilitoa agizo kwa Shekh Ponda kufika kituo cha polisi kutokana na kauli alizozitoa juu ya sakata la Tundu Lissu.

NAOT%203%20%281%29.jpg

Alichokiandika Halima Mdee twitter
 
Mwambie ajikite jimboni kwake kuleta maendeleo huku Kawe hali ni mbaya sana barabara zina mashimo ya kutosha tu!
 
Mwambie ajikite jimboni kwake kuleta maendeleo huku Kawe hali ni mbaya sana barabara zina mashimo ya kutosha tu!
Kazi ya mbunge ni kusimamia serikali,na kupeleka matatizo ya wanainchi wake na kupitisha sheria.kazi ya serikali ni kuleta maendeleo sehemu husika bila kujali itikadi.
 
Barabara zote za Dar ni mbovu. Wewe unaongelea kawe kuzuri namna hiyo?. Uje mwananyamala, nenda manzese, buguruni, ilala, kote kunakoishi watu wa kawaida Dar. Ni hatari. Wakati RC anachangisha fedha za nyumba za walimu hali ya barabara ni mbovu kabisa sehemu zote Dar isipokuwa upande wa baharini-oysterbay, masaki, bahari beach, salasala, nk.
Na hii ni kazi ya seriki siyo Mbunge. Usitudanganye wapiga kura.
 
Mapolisi buana.. kweli nimeamini akili yao ndogo sana.. mtu akiwa na kacheo ka hisani anafikiri kawa mungu.. ujinga mtupu.. hata sheria hayajui.. kazi kutumia miguvu tu. Huyo afande sirro kuonesha kuwa ni mweupe kichwani kuhusu sheria, hajui hata sheria gani inampa mamlaka gani kutamka alilolitamka.. hopeless kabisa

Tanzania hawajainunua na wala hawana hati milki.. kuongea jambo lolote ni haki yetu na hakuna mtu, bashite, [HASHTAG]#sizonje[/HASHTAG] au ku/ku mwingine aweza kuondoa haki hii.. hizo bhange wanazopiga zinawafanya kutojielewa

Ova
 
Kawe tunataka barabara
Mbunge ndie anawakusanyia kodi na kutafuta waandarisi? Poleni mnsowachagua Wabunge ili wawajengee barabara na kuwaondolea umasikini. Mkapa alisema mtaji wa masikini ni nguvu zake, ninyi mnaona wanasiasa ndio mtaji!

Vv
 
Mwambie ajikite jimboni kwake kuleta maendeleo huku Kawe hali ni mbaya sana barabara zina mashimo ya kutosha tu!
Nenda kaonane na mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni anayo bajeti ya kazi hiyo. Kabla ya kumwona mkurugenzi unaweza ukaanzia kwa mhandisi wa manispaa anaweza kukusaidia!
 
Back
Top Bottom