Halima Mdee: 'Nimekula bata' rumande

Halima Mdee: 'Nimekula bata' rumande

Halima Mdee alikuwa sero siyo jela maisha ya jela unayajua wewe, huko sero ndiyo alikula bata kutoka kwa nyampara.

Kuna wakati nakuona IQ yako iko juu sana na unafaa kwa mijadala lakini wakati mwingine (kama huu) inashuka below zero. Au ndio yale mambo ya ID ya ofisi kuwa kwa sasa anayetumia ID hii ya Ritz sio yule senior bali ni intern? Anafanya majaribio kabla ya ajira? Pse mkuu Ritz (original) ukiingia kazini tufahamishe maana kijana uliyemuachia anakufedhehesha.
 
Last edited by a moderator:
Anachomaanisha ni kwamba wanaojifanya wanatumia polisi kama wamewakomoa kumbe sio, wenzio ndo wanakomaa kama Mandela, sio kula kulala kama Riz1 kikwete, wanaopewa uongozi kama wa kifalme, watu wakipelekewa baiskeli wanahisi ndo maendeleo!
 
Amavubi

Halima annawabipu atawala.
Naona hata polosi walikuwa relaxed walipompeleka selo.

Ajue kuwa safari ijayo atajutia.
 
Last edited by a moderator:
Halima Mdee ana miaka 35 bado hajaolewa? Au sio wife matirial?
 
Huu ulikuwa ujumbe kwa wale ambao wakifikiri kumlaza segerea kutamnyongonyesha , aliwaambia kuwa yeye alikula bata n yuko tayari kurudi huko next time ........huu ujumbe utawauma sana waliofikiri kuwa kumpeleka segerea ni kumkomoa .......anawaambia yuko tayari kurudi tena Segerea .

Ukweli ni kuwa Askari wengi nchini kwa Sasa wanataka mabadiliko ( ya kura ) ...Ndio maana usitegemee kiongozi wa upinzani akienda Magereza atanyanyasika ......Hao Magereza wenyewe mnataka wafanyeje...wanadai malimbikizo,nyumba Zao mbovu ,sare Zao na Viatu ambazo ni haki wapate Jozi angalau mbili kila mwaka ...wengi wana miaka minne hawajapata...na kuna Askari wanavaa viraka ...wana raha gani ?? Sana Sana. Wanafanana na Hao wafungwa wanaowalinda ambao nao NGuo Zao ni midabwada...

Kwa taarifa tu ..au kukumbushana..CCM mwaka 2010 ...ilipata kura pungufu maeneo yote yenye makambi ya vyombo Vya Ulinzi na Usalama ....,hadi Kijitonyama wanakokaa walio nyumba kubwa ...that was a clear message kuwa nao wanataka kuboreshewa mazingira ya kazi...na pengine Hii imeongeza KASI YA SERIKALI KATIKA KUBORESHA MAISHA KWENYE MAKAMBI YOTE YA JESHI ...UJENZI WA NYUMBA MPYA UNAENDA KWA KASI
 
Hata mimi simuelewi labda ambaye hajawahi kwenda segerea hivi kukaguliwa kwa kuvuliwa nguo zote na kubaki kama mnyama ndo bata tena mbele za watu wengine? Kujisaidia kwenye ndoo lazima kwa mahabusu mgeni na mfungwa mgeni hilo ni bata?

Kulala sehemu sio salama kwani kuna mchanganyo wa watu mbalimbali wenye matatizo ya afya kama Tb hilo ni bata?

Nilijua akitoka atetea hali hatarishi ya maambukizi kule segerea yeye anasema bata.Kweli nimeamini do not trust anybody!!??
 
Ujue askali magereza wengi ni wafugaji wa bata inawezekana alipewa nyama ya bata ujue
 
Kamanda yeyote mkakamavu kama Mh Halima Hawezi kutishwa na sero za Tanzania zilizojaa wapiga kura wake .
 
sa mbona katoka si aendelee kula bata tu. Chezea bata..
 
tatizo la r na l linakuwa kubwa sana..?

Yaani wee acha tu,ingekuwa katika mazungumzo ya kawaida nikiwa na maana ya kutamka kwa kinywa hapo sawa ,kwani hapo unaweza kukosea ,lakini hata kuandika ,sijui tatizo ni nini? yaani wapo wengi kweli siku hizi,hata waandishi wa habari nao ni hivyo hivyo,duuh kazi kweli kweli.
 
kwa hiyo nanyi mnaanini kwamba segerea kuna kula bata labda kama ametumia tafsida ila there is no way kwamba lupango kuwe na raha zaidi ya uraiani na kama ni kweli watu watapangafoleni kwenda kula bata

Unabisha? Nenda kaombe kulala Segerea siku moja tu!
 
Ngoja nami nifanye fujo nikale bata Segerea. Nikifika tu kule nitakuwa napiga muziki na Babu Seya na kutunga nyimbo za kuikashifu serikali iliyopo madarakani kwa sasa.
 
ni kweli kim nana na siku hizi linakuwa kubwa hasa kwenye kuandika..

Wanakimbia somo la kiswahili shuleni..matokeo ndo haya...

Wengine matumizi ya h pia mtu anaandika uko badala ya huko, kipindi cha nyuma tatizo la r na l lilikuwa kwenye matamshi lakini kwenye kuandika watu walikuwa wanaandika ipasavyo but siku hizi ugonjwa umezidi mpaka na kwenye kuandika na kuzidisha ukubwa wa tatizo
 
Yaani wee acha tu,ingekuwa katika mazungumzo ya kawaida nikiwa na maana ya kutamka kwa kinywa hapo sawa ,kwani hapo unaweza kukosea ,lakini hata kuandika ,sijui tatizo ni nini? yaani wapo wengi kweli siku hizi,hata waandishi wa habari nao ni hivyo hivyo,duuh kazi kweli kweli.
Hii ya kwenye kuandika inanitatiza sana, sijui tatizo ni nini.?
 
Wengine matumizi ya h pia mtu anaandika uko badala ya huko, kipindi cha nyuma tatizo la r na l lilikuwa kwenye matamshi lakini kwenye kuandika watu walikuwa wanaandika ipasavyo but siku hizi ugonjwa umezidi mpaka na kwenye kuandika na kuzidisha ukubwa wa tatizo
Nafikiri pia linachangiwa na ubovu wa elimu yetu..
 
Back
Top Bottom