Halima Mdee: 'Nimekula bata' rumande

Halima Mdee: 'Nimekula bata' rumande

king suleman

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
1,749
Reaction score
1,151
Za jioni wana JF leo wakati na watch ITV habari kuhusu ile ishu ya Halima Mdee da yule dada kanichosha nikajikuta na cheka ni pale aliposema eti bata alilokula huko (sero) amekula bata ambalo hajawah kula uraiani nikastuka kidogo, Bata gan KWA ALIYE ANGALIA ANACHUKULIAJE HYO AU NI KUJIFARIJI


halimambaroni_300_183.jpg


MWENYEKITI wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee (35) na wenzake wanane wameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mdee na wanachama wengine wanane waliachiwa jana mchana baada ya kutimiza masharti.

Masharti hayo yalikuwa kusaini hati ya dhamana ya Sh milioni moja na kuwa na wadhamini wawili; mmoja awe mfanyakazi wa taasisi inayofahamika, awasilishe barua ya muajiri na kutambulisho cha kazi.

Baada ya kuachiwa, Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe, alisema; "walifikiri kunilaza Segerea siku moja wamenikomesha, nimekula bata ambayo sijawahi kula, na walioamua kuficha barua za dhamana wajue kama tulikuwa tunachechemea sasa tunakimbia".

Mdee na wenzake walifikishwa mahakamani hapo juzi na kusomewa mashitaka mawili ya kutotii amri halali ya Polisi na kufanya mkusanyiko usio halali.

Walipelekwa rumande kwa kuwa upande wa Jamhuri ulikuwa haujamaliza kukagua barua za wadhamini.

Washitakiwa hao wanadaiwa Oktoba 4, mwaka huu, katika mtaa wa Ufipa, bila kuwa na uhalali hao walikiuka amri halali ya kutawanyika iliyotolewa na Mrakibu wa Polisi (SP), Emmanuel Tillf kwa niaba ya Jeshi la Polisi.

Katika mashitaka mengine, inadaiwa siku hiyo katika eneo hilo, washitakiwa hao kwa pamoja, walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kutembea kwenda kwenye Ofisi ya Rais.
Walisomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Kaluyenda. Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Rose Moshi (45), Renina Peter maarufu kama Lufyagila, Anna Linjewile (48), Mwanne Kassim (32), Sophia F angel (28), Edward Julius (25), Martha Mtiko (27) na Beatu Mmari (35).

Upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na itatajwa tena Oktoba 21 kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.
CHANZO: Habari Leo
 
Hakuna kujifariji,ukweli ni kwamba naamin askar mag wanaunga harakat,ila tu wapo under order,bata itakuwa alikula tuuu!
 
kwa hiyo nanyi mnaanini kwamba segerea kuna kula bata labda kama ametumia tafsida ila there is no way kwamba lupango kuwe na raha zaidi ya uraiani na kama ni kweli watu watapangafoleni kwenda kula bata
 
Heheheee... Labda zile raha za "tachi ze wall"
..lol
 
Vyombo mbalimbali vya habari vimenukuu kauli iliyotolewa na Mh Halima Mdee akisema kwamba amekula bata alipokuwa mahabusu kuliko hata anavyokula bata uraiani

wenzangu mumemuelewa?


  1. anataka kutuaminisha kwamba huko mahabusu wanakula bata?
  2. huenda alipata nafasi ya upendeleo?
  3. je si hawa kwenye hotuba za bajeti wanaosema hali ya magerezani ni ngumu?
  4. Kauli hii inaweza kutafsiriwa vipi na mahabusu wengine?


Natafakari tu...
 
Vyombo mbalimbali vya habari vimenukuu kauli iliyotolewa na Mh Halima Mdee akisema kwamba amekula bata alipokuwa mahabusu kuliko hata anavyokula bata uraiani

wenzangu mumemuelewa?


  1. anataka kutuaminisha kwamba huko mahabusu wanakula bata?
  2. huenda alipata nafasi ya upendeleo?
  3. je si hawa kwenye hotuba za bajeti wanaosema hali ya magerezani ni ngumu?
  4. Kauli hii inaweza kutafsiriwa vipi na mahabusu wengine?


Natafakari tu.......
Huu ulikuwa ujumbe kwa wale ambao wakifikiri kumlaza segerea kutamnyongonyesha , aliwaambia kuwa yeye alikula bata n yuko tayari kurudi huko next time ........huu ujumbe utawauma sana waliofikiri kuwa kumpeleka segerea ni kumkomoa .......anawaambia yuko tayari kurudi tena Segerea .
 
Kwa ufafanuzi mwepesi badala ya kuachiwa juzi kwa dhamani dola iliamua aende lupango!
 
hiv hamjui kama maeneo ya magereza wanafuga bata weng so nafikir walimchinjia wa kutosha akala......

nwei la msing nafikir alimaanisha huko alikutana na watu wenye shida na yeye zaid na akapata nafas ya kua nao kwa karibu...
 
Ule ni usemi wa kisiasa zaidi kwa wanaoelewa. Kwani kula bata ni nini? Ni kufurahi na Mdee alifurahi maana alipata nafasi ya kukutana na watu ambao hangeweza kupata nafasi hiyo ya kukutana nao.
Hiyo ni misemo ambayo kwa sasa ndio inafahamika na idadi kubwa ya vijana ambao ndio wengi na nguvu ya chama. Mbona hakuna anayeuliza hapa kuwa jee alichinjiwa bata? Ni kwa vile wameelewa bata ni nini.
 
Vyombo mbalimbali vya habari vimenukuu kauli iliyotolewa na Mh Halima Mdee akisema kwamba amekula bata alipokuwa mahabusu kuliko hata anavyokula bata uraiani

wenzangu mumemuelewa?


  1. anataka kutuaminisha kwamba huko mahabusu wanakula bata?
  2. huenda alipata nafasi ya upendeleo?
  3. je si hawa kwenye hotuba za bajeti wanaosema hali ya magerezani ni ngumu?
  4. Kauli hii inaweza kutafsiriwa vipi na mahabusu wengine?


Natafakari tu.......
acha kuzuka watu, nyie si mlifikiri mnamkomoa kumbe mnajikomoa wenyewe!! we uliona wapi katiba ikatungwa na kundi moja ndani ya nchi - huo si ni uhalamia wa nchi kavu.
 
Back
Top Bottom