kibokilimani
Senior Member
- Jul 5, 2020
- 144
- 37
Halima amekuwa akiwapeleka sana pupa viongozi wake na kutowaheshimu na wakati mwingine kuwatukana kwa kweli hii ni kuonyesha kuwa amechoka na hawez lkn nikuforce kwa masilahi binafsi ya watu wachache wa chama .Taarifa za uhakika na za kweli nilizozipata ni kwamba Halima Mdee alikuwa hajajiandaa na hakuwa tayari kutuwakilisha sisi wananchi wa Kawe kama mbunge wa kuchaguliwa.
Ndio maana kwenye vikao vya ndani vya chama ilibidi Mwenyekiti Mbowe na katibu Mnyika wambembeleze sana na kumuomba afute maamuzi yake hayo.
Hii ilitokana na yeye mwenyewe kujitathimini na kuona hana cha maana cha kutuambia sisi wananchi wa Kawe na tukamuelewa kwa kuwa ahadi zote alizozitoa kwa miaka kumi yote hamna hata jambo moja lililokamilika. Ndo maana akaona ni heri akimbilie kwenye viti maalumu ili asiwe na mzigo wa kutuwakilisha sisi wananchi.
Nimejiuliza tu kama mtu hakuwa na utayari hadi kalazimishwa kutuwakilisha wananchi tuna uhakika gani na ahadi zake anazozitoa kwa sasa kama tu kwa miaka kumi alishindwa na alikuwa hajalazimishwa.
Amekuwa akifanya makosa mengi ndani ya chama lkn hakuwa anachukuliwa hatua kwasababu bado wanataka kumtumia kuwakandamiza wananchi na kuyalisha matumbo yao. Nakujifanya wanauchungu yani mwizi hana rangi niwaulize halima amepeleka hela za halmashauri na misaada ya mashirika binafsi wap kwa miaka mitano tu wala tusiongelee miaka 10