Halima Mdee kikaangoni live ya EATV

Halima Mdee kikaangoni live ya EATV

me4u

Member
Joined
Oct 26, 2012
Posts
42
Reaction score
13
Yaani hawa washikaji kama walijua vile huyu mdada nina maswali kibao sana juu yake.

Awamu hii ya pili ya uongozi wake huku Kawe naona kama amelegea tofauti na pale mwanzo,nimeicheki hii nikaona nishee na na nyie wadau wenzangu, maana hii wanasema unamuuliza swali naye anakujibu katika comment yake.

Itakuwa Jumatano ya kesho kuanzia saa 6 mchana kwenye page yao ya facebook eatv.
 
Attachments

  • kikaangoni-halima.png
    kikaangoni-halima.png
    38.2 KB · Views: 302
hakuna jipya alilotufanyia wana cow way kama kuna aliyeona alichofanya a comment
 
Si umesema kesho atakuwa hewani? Tumwone kesho atakachotuambia na tuwe tayari kumrushia maswali. Atuambie amefanya nini na amepanga kukamilisha nini kabla ya uchaguzi ujao. Isitoshe na sisi tujiulize tumefanya nini kubadilisha hali ya familia zetu kuanzia elimu, afya, usafi, usalama na makazi. Je umelipa kodi ya ardhi? Umelipa kodi ya majengo? Kama umelipa una haki ya kudai maendeleo katika jimbo lako.
 
watu bwana kwa lawama,huyu dada kaongoza kawe mda mfupi,mbona ccm wameongoza miaka zaid ya 30 na hamkulalamika??
 
Huwezi kuhukumu kwa macho na akili tungoje kesho atajibuje maswali na yale mabo atakayokuwa hajayafanya atatueleze kwanini ameahundwa kuyanfanya point hiyo
 
Yaani hawa washikaji kama walijua vile huyu mdada nina maswali kibao sana juu yake.

Awamu hii ya pili ya uongozi wake huku Kawe naona kama amelegea tofauti na pale mwanzo,nimeicheki hii nikaona nishee na na nyie wadau wenzangu, maana hii wanasema unamuuliza swali naye anakujibu katika comment yake.

Itakuwa Jumatano ya kesho kuanzia saa 6 mchana kwenye page yao ya facebook eatv.

Awamu ya pili ya uongozi wake unamaanisha nini? Kwamba kabla ya kuwa Halima Mdee hapo awali alikuwa anajiita Ritha Mlaki?

Kawe tuna bahati mbaya ya kupata wabunge wanawake wasiowajibika ipasavyo. Kama ambavyo sijaona Ritha Mlaki alichofanya ndivyo ambavyo sioni anachofanya Halima Mdee huku Kawe.

Tuna bahati mbaya sana wana Kawe. Ntajaribu kugombea na mimi nione.
 
Back
Top Bottom