Hata kama ni mambo ya kisiasa,twende taratibu. Jana, Mbunge wa Kawe (CHADEMA) na Mwenyekiti wa BAWACHA
Halima Mdee alikosa dhamana na kuswekwa rumande. Ikatolewa sababu kuwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana. Sasa, hebu twende hatua kwa hatua.
Kwanza
Halima Mdee alikamatwa. Pili
Halima Mdee akaachiwa kwa dhamana ya Polisi. Tatu
Halima Mdee alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka yake. Nne, upande wa Mashtaka haukuwa na pingamizi juu ya dhamana ya
Halima Mdee wala wenzake. Tano,Hakimu akatoa masharti ya dhamana. Sita, washtakiwa wote walikuwa tayari kuyatekeleza na kuachiwa kwa dhamana. Saba, upande wa Mashtaka ukataka kwenda kuhakiki wadhamini wa
Halima Mdee na wenzake.
Umepagundua penye tatizo? Ni hapo pa kuhakiki wadhamini.
Halima Mdee anajulikana. Wadhamini wake, ambao wengi ni Wabunge na Maafisa wa CHADEMA Makao Makuu wanajulikana. Kuhakiki kulikujaje? Wengine mbona hawafanyiwi hivyo? Kibaya zaidi,wahakiki hawakuenda mahali popote hadi
Halima Mdee alipopandishwa karandinga na kwenda mahabusu. Wahakiki walitokomea kusikojulikana. Why?........Kwanini?
Nitoe rai kwa wahusika wote kufanikisha dhamana ya
Halima Mdee. Ingawa si wa chama changu, hastahili kombolela lililochezwa jana. Hakuna haja ya 'kuipaisha' CHADEMA na viongozi wake kupitia Mahakama. We are suffering from that;it must end! Pole sana
Halima Mdee.
Updates....
Halima Mdee na wenzae 8 wamepata dhamana. Ni jambo jema
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam