VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Hata kama ni mambo ya kisiasa,twende taratibu. Jana, Mbunge wa Kawe (CHADEMA) na Mwenyekiti wa BAWACHA Halima Mdee alikosa dhamana na kuswekwa rumande. Ikatolewa sababu kuwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana. Sasa, hebu twende hatua kwa hatua.
Kwanza Halima Mdee alikamatwa. Pili Halima Mdee akaachiwa kwa dhamana ya Polisi. Tatu Halima Mdee alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka yake. Nne, upande wa Mashtaka haukuwa na pingamizi juu ya dhamana ya Halima Mdee wala wenzake. Tano,Hakimu akatoa masharti ya dhamana. Sita, washtakiwa wote walikuwa tayari kuyatekeleza na kuachiwa kwa dhamana. Saba, upande wa Mashtaka ukataka kwenda kuhakiki wadhamini wa Halima Mdee na wenzake.
Umepagundua penye tatizo? Ni hapo pa kuhakiki wadhamini. Halima Mdee anajulikana. Wadhamini wake, ambao wengi ni Wabunge na Maafisa wa CHADEMA Makao Makuu wanajulikana. Kuhakiki kulikujaje? Wengine mbona hawafanyiwi hivyo? Kibaya zaidi,wahakiki hawakuenda mahali popote hadi Halima Mdee alipopandishwa karandinga na kwenda mahabusu. Wahakiki walitokomea kusikojulikana. Why?........Kwanini?
Nitoe rai kwa wahusika wote kufanikisha dhamana ya Halima Mdee. Ingawa si wa chama changu, hastahili kombolela lililochezwa jana. Hakuna haja ya 'kuipaisha' CHADEMA na viongozi wake kupitia Mahakama. We are suffering from that;it must end! Pole sana Halima Mdee.
Updates....
Halima Mdee na wenzae 8 wamepata dhamana. Ni jambo jema
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Last edited by a moderator: