Wana JF wenzangu, mimi ni intetested party kwenye mgogoro huu kwa sababu ni mmoja wa wamiliki wa mashamba eneo hilo.
Japo siungi mkono kilichotokea, chanzo ni jamaa wanaojiita madalali huku wakikingiwa kifua na serikali ya mtaa kuruhusu wavamizi kuvamia maeneo ya watu na kujenga makazi yao. Just imagine una shamba lako siku ya siku mtu anajitokea alikotokea na kujenga shambani kwako huku serikali ya mtaa ikitazama!.
Siungi mkono mmoja wa wamiliki hao kukodisha mabaunsa lakini pia siungi mkono serikali ya mtaa kuwakingia kifua wavamizi hao.
Mgogoro huu ndio mtihani mkubwa kabisa wa mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee ambaye amelikwaa jimbo hilo kwa kutumia kura za matumaini ya wavamizi hao kuwa atasimama nao mpaka mwisho huku akijua wazi they are simply wavamizi?.
Serikali ya kijiji imewaacha wanakijiji wake kuuza mashamba kwa watu wachache, sasa maeneo ya kuuza yameisha, serikali ya mtaa ina wahamasisha wanakijiji hao kujitwalia tena maeneo yale yale waliyoyauza.
Naamini kwa dhati kuwa Mhe. Mdee anakijua vizuri sana kinachoendelea, naomba asizidi kutoa false hopes kwa wavamizi hao kama shukrani kwa kura, ni bora sasa awaambie kampeni zimepita, yeye ni mbunge wao lakini its high time wafuate sheria, taratibu na kanuni. Rungu, panga na shoka sio miongoni mwa taratibu za umilikaji ardhi.