Halima Mdee atelekeza mwanachama Polisi Mabwepande

Halima Mdee atelekeza mwanachama Polisi Mabwepande

Volodimiri Zelensiki

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2015
Posts
1,460
Reaction score
4,524
Chadema ni wapiga dili, Halima Mdee na kina Boniface Jacob ni wahuni kama wahuni wengine. Haiwezekani leo ni siku ya Tano tangu mwenyekiti wa Boko Basihaya ashikiliwe na polisi bila nyie kuonekana na bila kupelekwa mahakamani. Ni wazi raia wa nchi hii hawategemei kupata haki kwa jeshi la polisi kwa sababu mbalimbali za kutumika kisiasa.

Katika hali ianyoonyesha chadema sio chama ila ni Genge Maslahi wamemtelekeza mwenyekiti wa mtaa wa Boko Chasimba/Basihaha ndugu Marinos Mwandule kwa kosa la kuzozana na maafisa wa TASAF waliokwenda mtaani hapo usiku wa Alhamisi iliyopita kwa malengo yasiyojulikana.

Kuonesha kwamba kukamatwa kwa mwenyekiti huyu kupitia Chadema ni mpango uliosukwa kijinga na diwani wa kata ya Wazo bwana Majisafi maafisa hao waliokuwa na kikundi cha wanausalama walivamia mtaa huo kwa nia ya kumkamata Ndg. Marinos Mwandule kwa kujifanya ni maafisa TASAF hata hivyo baada ya diwani akiongozana na polisi kufika ndipo ilipobainika kwamba lile lilikuwa genge la wasiojulikana na kwa mujibu mashuhuda wa tukio hilo. Hii ni siku ya Tano tangu mwanachama huyo kutiwa nguvuni bila kufikishwa mahakamani.

Kwa hali hii Chadema ni wahuni wasikabidhiwe nchi wala mtaa. Kwa wenyeji wa boko basihaya huu ni wakati wa kukipa fursa chama cha mapinduzi ili kitetee wananchi na sio wahuni Chadema wanaojali matumbo yao. huu ni wakati wa bwana Marinos kurudisha kadi ya Chadema na kujiunga rasmi na chama cha mapinduzi ili kuunga juhudi za kuleta maendeleo mtaani hapa.
 
Huruma hiyo ungeitumia kuwashirikisha CHADEMA kufuatia hilo swala. Unalaumu kana kwamba jeshi la polisi ni la CHADEMA.
Ebu chitathmini ni wazi unajiuza kwa maccm Yaani huna uutu ni malaya fulani.
 
Ila mwanzisha mada wewe sio Chadema bana ....alafu unajuaje chama kinafuatilia hili maana si lazima Mdee na Jacob wawepo kila tukio mtawalaumu bure
 
Aisee ...kwanini wazungu waliondoka Tanganyika.. Yaani CCM mnashirikiana na polisi kuwakamata makamanda wa CHADEMA alafu mnakimbilia mitandaoni kulaum kuwa CHADEMA mpaka sasa hawajafika polisi. Pole sana...ILA MALIPO NI APA APA
 
Mkuu swali zuri Sana huwa nawaambia vijana Chadema ni chama Cha kikabila wanabisha wanafikiri kuwa mwanaharaki ni lazima uwe Chadema hapa ndio huwa nawaelewa Ccm

Sasa Mdee hapo ana nguvu gani kumtoa huyomtu huko Jela. Mtu anayetesa wananchi mnamjua na huyo mleta uzi ndie anayemtetea mtesi.Watu mana vichwa vya ajabu ssna. Halafu hao watesi siku wakikugeukia tusisikie unatoamlio nyambaf
 
Mkuu swali zuri Sana huwa nawaambia vijana Chadema ni chama Cha kikabila wanabisha wanafikiri kuwa mwanaharaki ni lazima uwe Chadema hapa ndio huwa nawaelewa Ccm

Kwa kuwa nedula oblongata yako ni uji wa mahindi nakusamehe bure
 
Mkuu mbona umehitimisha ya kuwa tuwape kura ccm na wala sio chama chengine kama vile cuf,tlp,nccr mageuzi n.k,je? Tukisema ccm ndio imefanya huu upuuzi kwa kuogopa kushindwa na huyo jamaa kwenye uchaguzi tutakuwa tumefanya makosa.
Nalog off
 
Mkuu swali zuri Sana huwa nawaambia vijana Chadema ni chama Cha kikabila wanabisha wanafikiri kuwa mwanaharaki ni lazima uwe Chadema hapa ndio huwa nawaelewa Ccm

Hamna sera za kutueleza, mbona ukijiunga na hicho chama chenu inabaki a na hoja dhaifu kama ukabila, udini ukanda. Hizo ndio sera zenu? Mmesahau ile ya watu wenye mawazo mbadala wataleta vita na watakao adhirika zaidi ni watoto na Wanawake , poor CCM
 
Mtoa mada nahisi kichwani ana uji wa ulezi , hana ubongo.

Diwani wa CHADEMA amekamatwa na polisi wa Jamhuri halafu analaumiwa Halima Mdee na Boniface Jacob kwa nini huyo mtuhumiwa hajapelekwa mahakamani.

Dah! Hiki ni kituko cha karne kabisa. Sasa polisi wanakamata RAIA hawawapeleki mahakamani wanasubiri viongozi wa upinzani wawakumbushe. Damn bullshit!!!!

Hii mbinu uliyotumia kuhamasisha hao nzi wa kijani haina mashiko jaribu nyingine.
 
Back
Top Bottom