Elia F Michael
Member
- Mar 3, 2018
- 75
- 799
Siku ya Jumamosi Tar 26 January 2019 Polisi Katika Kijiji cha Mganza Kata ya Kanyonza Wilaya Kakonko waliua watu 8 waliodhaniwa kuwa ni majambazi.
Polisi walipokea taarifa ya kutekwa kwa mtoto katika kijiji hicho,huku watekaji wakishinikiza kupewa fedha ili wamuachie mtoto vinginevyo watamuua.
Polisi waliamua kwenda kwenye kijiji hicho kufanya doria hadi mashambani,wakawapiga watu 8 risasi wakawa wamekufa wakidhani kuwa ndio majambazi.
Wamewazika kwenye shimo moja Kijiji cha Mganza siku ya Jumapili Tar 27 January 2019.
Polisi wao wamesema walipambana nao.
Lakini taarifa kutoka kijiji cha Mganza zinadai kuwa Polisi wamewaua watu hao wakiwa wanalima shambani. Vijiji vya Mpakani Kigoma vina utaratibu wa Kisheria wa kuwatumia Raia wa Kigeni kutoka Burundi Kuja kufanya kazi kama vibarua kupitia ofisi za uhamiaji zilizopo Kakonko na Wilaya za Kigoma.
Baadhi ya wananchi wa Burundi wameanza malalamiko kuwa Ndugu zao waliotoka Burundi kuja Tanzania kama vibarua ndio wameuliwa na wako tayari kulipiza kisasi.
Nawasihi wananchi wanaoishi vijiji vya Kabare,Gwarama Mganza ,Muhange,Nyakayenzi,Kasongati,Kikulazo,Bukililo,Gwanumpu,Mgunzu na Kiduduye kuwa makini na kuishi kwa Tahadhari.
Nimetoa Taarifa Polisi na Mkuu wa Wilaya pia nimemueleza.
Hili jambo nimewaomba lifanyiwe kazi vinginevyo tutapata doa chafu kimataifa huku Maisha ya wananchi yakiwa hatarini kukumbwa na vita.
Mungu tulehemu.
Hata hivyo hata baada ya vifo vile watekaji wa Mtoto wameendelea kumshikilia mtoto hadi walipo pewa fedha.
Hii ina maana ya kwamba uwezekano ni mkubwa kwamba waliouliwa sio walioshikilia mtoto.
Sent using Jamii Forums mobile app