Hali ya usalama wa mpaka wa Tanzania na Burundi unaweza kuwa kwenye hatari ya mgogoro kufuatia mauaji ya watu 8 Kakonko

Mar 3, 2018
75
799
Siku ya Jumamosi Tar 26 January 2019 Polisi Katika Kijiji cha Mganza Kata ya Kanyonza Wilaya Kakonko waliua watu 8 waliodhaniwa kuwa ni majambazi.

Polisi walipokea taarifa ya kutekwa kwa mtoto katika kijiji hicho,huku watekaji wakishinikiza kupewa fedha ili wamuachie mtoto vinginevyo watamuua.

Polisi waliamua kwenda kwenye kijiji hicho kufanya doria hadi mashambani,wakawapiga watu 8 risasi wakawa wamekufa wakidhani kuwa ndio majambazi.
Wamewazika kwenye shimo moja Kijiji cha Mganza siku ya Jumapili Tar 27 January 2019.

Polisi wao wamesema walipambana nao.

Lakini taarifa kutoka kijiji cha Mganza zinadai kuwa Polisi wamewaua watu hao wakiwa wanalima shambani. Vijiji vya Mpakani Kigoma vina utaratibu wa Kisheria wa kuwatumia Raia wa Kigeni kutoka Burundi Kuja kufanya kazi kama vibarua kupitia ofisi za uhamiaji zilizopo Kakonko na Wilaya za Kigoma.

Baadhi ya wananchi wa Burundi wameanza malalamiko kuwa Ndugu zao waliotoka Burundi kuja Tanzania kama vibarua ndio wameuliwa na wako tayari kulipiza kisasi.

Nawasihi wananchi wanaoishi vijiji vya Kabare,Gwarama Mganza ,Muhange,Nyakayenzi,Kasongati,Kikulazo,Bukililo,Gwanumpu,Mgunzu na Kiduduye kuwa makini na kuishi kwa Tahadhari.

Nimetoa Taarifa Polisi na Mkuu wa Wilaya pia nimemueleza.
Hili jambo nimewaomba lifanyiwe kazi vinginevyo tutapata doa chafu kimataifa huku Maisha ya wananchi yakiwa hatarini kukumbwa na vita.

Mungu tulehemu.

Hata hivyo hata baada ya vifo vile watekaji wa Mtoto wameendelea kumshikilia mtoto hadi walipo pewa fedha.
Hii ina maana ya kwamba uwezekano ni mkubwa kwamba waliouliwa sio walioshikilia mtoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Burundi silaha zinamilikiwa kiholela hivyo wawe makini kuanzia askari polisi wa maeneo ya kijiji hicho mpaka Raia.
 
Fanya yote ila usicheze na mtu/watu waliozoea vita/ mapigano yani wao milio ya risasi kwao ni kama beat ya kwangwaru alafu wewe mwenzangu na mm ata ukisikia zile baruti za watoto wanapigaga kwenye mikesha ya mwaka mpya unajifungia chumbani tena mpaka uvunguni mwa kitanda. Chondechonde ndugu zangu wa kakonko uwo mziki nendeni nao taratibu.
 
Hapo sasa jeshi likipelekwa ndiyo mahali pake sahihi, sio kununua na kubeba korosho au kulinda maduka ya fedha za kigeni
 
Juzi kulikuwa na mada ya polisi kuua majambazi 8 Mwanza , nikasema hapa Hawa jamaa hawaaminiki, wanaweza kusema wameua majambazi then ndugu wanajitokeza kupinga. Baadhi walinikejeli.. Haya sasa, Leo ndio hayo hayo yametokea..
Ni ngumu kuwaamini Hawa jamaa siku hizi..
Sijui tunaelekea wapi??

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi huwa cwaamini kabisa polisi sababu kama mwanza wanasema wameua majambazi 8 na walikuwa na silaha na hakuna polisi alieshambuliwa hii haingii akilini kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi kulikuwa na mada ya polisi kuua majambazi 8 Mwanza , nikasema hapa Hawa jamaa hawaaminiki, wanaweza kusema wameua majambazi then ndugu wanajitokeza kupinga. Baadhi walinikejeli.. Haya sasa, Leo ndio hayo hayo yametokea..
Ni ngumu kuwaamini Hawa jamaa siku hizi..
Sijui tunaelekea wapi??

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo huko mwanza wamelalamika au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka wetu na Burundi una njia nyingi za panya zinazotumiwa na warundi kuingia nchini kutafuta vibarua. Kuanzia wilaya ya Kasulu, Kibondo na Kakonko pamoja na kuwa na vituo mahususi vya uhamiaji vya Manyovu, Mabamba na Nyabibuye, bado kuna njia za panya maeneo ya Munyegera Mugunzu na Muhange. Kwa hali ilivyo, hasa ukizingatia hali ya usalama ilivyo tete nchini Burundi, ni wakati sasa tunatakiwa kuwa na patrol za kijeshi katika mpaka wetu wa magharibi.

Kwa kupeana uzoefu tu, mwaka juzi nikitokea Bujumbura kwenye ofisi ya uhamiaji Makamba kwenye mpaka wetu na Burundi upande wa Burundi, nilikuta wamekamata warundi sita, waliokuja kufanya uhalifu upande wetu, wakafanikiwa kurudi upande wao bila kukamatwa na askali wetu, lakini wakaja kukamatwa na askali wa Burundi. Kwa kuwa nilikuwa nasubiri kugongewa mhuri wa kutoka na kusubiri gari la kunipeleka mpakani, niliweza kuipata stori yote jinsi walivyokuwa wakigombezwa waharifu hao.

Huo utaratibu wa kuruhusu kufanya vibarua kwa raia wa kigeni kwa mwavuli wa ujirani mwema, ungepitiwa upya na ikiwezekana uondolewe kwa kuwa unahatarisha usalama wa raia, hasa ukizingatia kuwa baadhi ya warundi wanamiliki silaha za kivita... ndio hao huwa wanateka mabasi ya abiria. Ulinzi uimarishwe!!
 
Mkuu usilolijua ni usiku wa giza. Tarehe 28/01/2019 majira ya saa mbili kasa robo maeneo ya Busunzu (katikati ya Kibondo na Kasulu)kuna utekaji wa gari la abiria kutoka Kagera to Kigoma.ulifanywa na haohao warundi wakiwa na SMG UZ moja na SMG AK 47 moja mapanga ya kutosha na marungu manne chakushukuru Mungu hakuna abiria aliyejeruhiwa ila waliporwa Mali zao, kifupi kwa sasa wamecharuka kwakuwa kuna mpango wa kuwarudisha kwao Burundi huenda wanatafuta mitaji.
 
Aliyezoea kula nyama ya binadamu kamwe hawezi kuacha,warudi walishaonja nyama ya binadamu bila kuwa nao makini raia waishio jirani na Burundi hawawezi kuwa na Amani ya kudumu
 
Back
Top Bottom