Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,869
- 828,391
Kilichokuwa kiwe uchaguzi mkuu Tanzania kwa mujibu wa katiba yake, kimepita na yaliyotokea sote tunayafahamu!
Bado taifa halijatulia, bado fukuto lipo, la dhuluma, la maumivu, la ukatili mkubwa uliitokea nknk
Hofu kwa upande wa pili ni kubwa zaidi.. Nadhani intelijensia inawapenyezea hali halisi... Ni lazima lifanyike jambo la maamuzi magumu sana kwa upande wao ili kuweza kutamatisha hii hali
Kamatakamata na utekaji unaoendelea havina afya kwa taifa bali vinazidisha uchungu na maumivu kwa yaliyokwisha tokea
Haya mambo yanazidisha usugu na kuzalisha uasi... Haitakaa itokee watu wanyamaze mazima kama matakwa yao ya kikatiba hayatatekelezwa
Kiasili binadamu amezaliwa kuongea, ni vigumu sana kumziba mdomo asiongee! Kwa kufanya hivyo unazalisha kitu kingine hatari zaidi
Wakosoaji waachiwe waongee ndio njia pekee iliyobaki ya kuwapunguzia maumivu na fukuto mioyoni mwao! Haitakaa itokee kuwanyamazisha wote kwa kuwateka, kuwapoteza, kuwatesa, kuwabambikia kesi kubwa zisizo na dhamana ama kuwaweka kizuizini kwa kesi ghushi
Kufanya hivyo hakuleti suluhu bali kunaongeza tatizo ambalo siku likikomaa tufani yake itakuwa na mshindo mkubwa sana!
Ukiwabufaza waliopo kwa mbinu mbalimbali kuna kundi lingine kubwa nyuma yao litaibuka. Ambalo ni
Kubwa zaidi
Baya zaidi
Kwaweli tumechoka kuzika, tumechoka kupoteza ndugu jamaa na marafiki,
Tumechoka kuhudhuria kesi za michongo
Kutibu majeraha na majeruhi wa ukatili vituo vya police
Wahanga ni wengi sana na kila mhanga ana chain ya watu wasiopungua 20! Mnadhani tunalipeleka wapi taifa
Taifa linaingia kwenye mdororo mkubwa wa kiuchumi.. Madhara yake yataonekana mwakani.. Badala ya kuwekeza kwenye umoja wa kitaifa ili nguvu kazi iliyopo itumike kwenye uzalishaji.. Tumewekeza kwa machawa na kutaka kufubaza nguvu kazi hiyo! Je mnadhani tutafika?
Tunatumia muda mwingi na rasilimali kuwinda watu
Tunatumia muda mwingi na rasilimali kuwateka
Tunatumia muda mwingi kuwatesa na kuwadhalilidha
Tunawaumiza kwa kuwasababidshia majeraha na ulemavu
Nao wanatumia muda mwingi kujitibu, kujiuguza na kuhudhuria kesi za mchongo.. Huu ni uhujumu uchumi
Tunazalisha yatima wajane na wagame bila kujua.. Familia zinasambaratika.. Breadwinners wengi katika familia ndio hao walioko kwenye madhila ya kila aina!
Je wenye hekima na uthubutu wameisha Tanganyika!?