Hali ya umeme nchini

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
13,602
9,157
Kuna uwezekano mkubwa pande mbalimbali za nchi zimekuwa zikiugulia maumivu ya kukosa umeme. Mimi natulia maeneo ya Gongolamboto. Hali ya umeme ni mbaya mno. Umeme unakatika hovyo wakati mwingine kwa masaa 12. Biashara nyingi zimeathirika kufuatia kukatika umeme karibu kila siku. Mbaya zaidi kwa kipindi cha wiki mbili sasa, kila ifikapo saa 2 usiku, kama umeme upo, TANESCO hubonyeza 'reset button' ambapo umeme hukatika na kuwaka hovyo kabla haujatoweka kabisa au kuwaka tena.
wakati waziri Muhongo anachukua madaraka alijigamba kwamba mgawo ulikuwa wa kutengenezwa na kuapa kuwa hautakuwepo tena. Au ndio tuseme kuwa na yeye ameingia kwenye pay roll ya wenye nchi?
 
Songoro

JF-Expert Member
May 27, 2009
4,124
1,012
Kama mleta uzi ni mfuatiliaji wa matukio ya kisiasa atajua ujanja wa wanasiasa, Wakati Zitto akishikilia bango ukiukwaji wa sheria ya Manunuzi ulofanywa na Muhongo na Katibu wake Bw. Maswa kwa ukuipa tenda Puma kwa mlango wa nyuma ili kuzuia au kututoa kwenye mjadala wa kupindishwa kwa sheria hii Prof MUONGO akajidai kusema mgao hautakuwepo tena, wale wabunge vichwa maji wakaanza kushangilia bila ya kuhoji uhalali na ukweli wa kauli hiyo,matokeo yake ndo haya na Zitto alisema bora awe mpweke wa muda kuliko kushabikia uongo! Mgao wa umeme haukomeshwi kwa matamko!
 
Mkuu wakati wa saga lile niliweka mada kujaribu kuonyesha mbinu chafu ya Muhongo na Maswi baadhi ya member humu wakadiriki kuniita eti ama mimi ni mbunge ama nina maslahi fulani pamoja na Zitto Kabwe. Nilikuja gundua kuwa tatizo lililopo kwa watanzania hata wa kada ya 'wasomi' ni MYOPIA.
 
Baba_Enock

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
7,032
2,290
Mgao wa umeme upo na unaedelea maeneo mengi ya Dar es Salaam yanapata umeme chini ya masaa 14 kwa siku...!
 
mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,548
6,671
Huyu Prof. Alikuwa anasinzia alipoamshwa akaulizwa vipi prof mgao hupo haupo akasema ni wewe wasema kwamba haupo
 
Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
13,602
9,157
Naona hata Badra Masoud amezikimbia media siku hizi. Maneno meeeengi, matendo kidogoooo. Tanzania kila mtu ni mwanasiasa, regardless yuko kwenye nafasi ya kisiasa ama la!
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
96,662
165,845
Hakuna cha Muhongo wala nini , kuna tetesi kwamba mgawo utaongezeka zaidi January , maneno matupu hayawezi kubadilisha lolote , bila ku create vyanzo vya uhakika vya uzalishaji wa umeme haitawezekana kupunguza hii shida , tuliambiwa baada ya songosongo gas kila kitu kitakuwa sawa , leo kiko wapi !
 
Je, huu waweza kuwa mojawapo ya ushahidi kuwa nchi inaendeshwa kisanii?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom