• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Hali ya Umaskini Tanzania yapungua kwa asilimia hizi, Mkurugenzi ofisi ya Takwimu Tanzania athibitisha hilo

KITAULO

KITAULO

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2018
Messages
1,055
Points
2,000
KITAULO

KITAULO

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2018
1,055 2,000
Imeelezwa kuwa takwimu za hali ya umaskini wa kipato hapa nchini kwa mwaka 2017, zimepungua kwa kiasi kikubwa na kufikia asilimia 26.


Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt Albina Chuwa
Hayo yamebainishwa leo Februari 17, 2020 na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt Albina Chuwa na kusema kuwa jukumu la kuondoa umaskini kwa mtu mmoja mmoja ni jukumu la watu wote.
“Hali ya umaskini wa kipato hapa nchini Mwaka 1991-92 ulikuwa Asilimia 39, 2007 umaskini ulikuwa asilimia 34, 2012 Asilimia 28.4 na 2018 hali ya umaskini likuwa 26.4, kasi ya kupungua umaskini hapa nchini inaenda kwa mwendo wa kasi” amesema Dkt Albina Chuwa Mkurugenzi wa Takwimu.
Aidha akitoa takwimu za umaskini kwa nchi zingine za Afrika Dkt Chuwa amesema,“Rwanda utafiti wao wa mwisho ulikuwa Mwaka 2015, na hali ya umaskini ilikuwa Asilimia 38.2, Kenya 2015 ni asilimia 36.3, Afrika Kusini Asilimia 55.5, Zambia Asilimia 54.4,na kwa mwaka huo huo Zimbabwe ilikuwa ni Asilimia 72.3, hii ndiyo hali ya umaskini ya mahitaji ya msingi kwa Nchi za Afrika”.

Hayo yamejiri katika uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF, mpango ambao utazinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

eti umaskini unapungua kwa kasi ya turbo...acha nicheke tu kama ni mazuri...🙃🙃🙃🙃🙃🙃🙃
 
Equipment

Equipment

Senior Member
Joined
Feb 14, 2017
Messages
186
Points
250
Equipment

Equipment

Senior Member
Joined Feb 14, 2017
186 250
Masikini Nchi yetu sijui tulikosea wapi yote hayo wanayaongea huku nafsi zikiwasuta ila tu wamfurahishe mwenye Nchi
 
KITAULO

KITAULO

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2018
Messages
1,055
Points
2,000
KITAULO

KITAULO

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2018
1,055 2,000
Uchumi unakuwa kila mwaka...asante mzee wa chato
 
Abou Saydou

Abou Saydou

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2014
Messages
2,643
Points
1,500
Abou Saydou

Abou Saydou

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2014
2,643 1,500
Watajijua wenyewe......takataka wanazopublish zinazidi kudumaza akili zetu.
 
Msingida

Msingida

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Messages
5,380
Points
2,000
Msingida

Msingida

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2010
5,380 2,000
Wana data za kupika,
Hali halisi ni kinyume chake
 

Forum statistics

Threads 1,402,685
Members 530,969
Posts 34,402,225
Top