Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,278
- 8,868
Bingwa wa zamani mara saba wa mbio za magari ya fomula one Michael Schumacher ameonesha hali ya matumaini kidogo leo baada ya operesheni ya pili .Madaktari wanaomfanyia upasuaji wamesema wamepata mafanikio jana usiku lakini bado yuko kwenye hali mbaya
Mkewe na watoto wawili wako katika hospitali hiyo mjini Grenoble nchini Ufaransa ambako dereva huyo wa zamani wa mbio za magari amewekwa katika hali ya bandia ya kuzimia, baada ya kupata maumivu makali baada ya kujigonga kwenye jiwe kichwani wakati akiwa kwenye mchezo wa kuteleza katika barafu siku ya Jumapili. Taarifa za ajali hiyo zimeushitua ulimwengu na madereva nyota wa mbio hizo wamejiunga na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel pamoja na mashabiki wa mchezo huo kuelezea matumaini yao kuwa atapata nafuu.