Hali ya Muhimbili na Uongozi wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali ya Muhimbili na Uongozi wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 24, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hospitali ya Muhimbili inategemewa na watu wengi na kutokana na umuhimu wake imekuwa ni hospitali ya rufaa si kwa mtindo wa kawaida bali pia kwa magonjwa ambayo yangeweza kuhudumiwa katika hospitali nyingine. Ninapoangalia suala la Health Reform ya Marekani ninajiuliza je tunahitaji kufanya mabadiliko katika sekta yetu ya afya na hasa kwa wakazi kama wa Dar?

  Je, hospitali ya Muhimbili na zile nyingine za wilaya zinakidhi mahitaji yetu?

  Je mapungufu yaliyopo sasa yanaweza kurekebishwa au ndio tukubali kuwa "hali ndivyo ilivyo"?

  Je, kiongozi kama Kikwete ana maono ya kubadilisha mfumo wetu wa afya ili uwe people friendly, affordable na zaidi ya yote uwe ni bora katika huduma au na yeye amekubali kuwa "hali ndivyo ilivyo"?

  Je, tumekuwa tunaalika wawekezaji katika maeneo mengi (makubwa hasa mawili, madini na utalii) kwanini hatujafanya jitihada ya wazi na kuvuna uwekezaji katika sekta ya afya kwa sababu zilezile na hata kubinafsisha baadhi ya hospitali ili ziendeshwe kibiashara na kiushindani?

  Je, katika mipango yetu ya afya kwanini Taifa la Tanzania halina Hospitali hata moja maalum ya Rufaa kwa ajili ya watoto na magonjwa ya watoto?

  Kiufupi nauliza unatosheka na mfumo wetu wa afya ulivyo sasa au hutosheki? Kama kuna mabadiliko ungependa yawepo ambayo yangehakikisha kufikika kwa urahisi, gharama nafuu na huduma bora na ya wakati ni mabadiliko gani hayo?

  Je na wewe ni muumini wa imani ya kwamba "hali ndivyo ilivyo" na hivyo tujifunze kuishi kwa kile kilichopo na tusijaribu kukibadilisha tusije tukaonekana tunataka kuishi kama wazungu!?
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Mar 24, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Mimi sitosheki na mifumo karibu yote tuliyonayo. We are a pathetic bunch! Mabadiliko ni ya lazima ktk nyanja zote-kifikra, kielimu, huduma za afya, haki, usalama, uchumi, siasa, na mengineyo mengi tu

  Hali sivyo ilivyo. Ni sisi watu tunaofanya hali iwe namna moja ama ingine. Kwa hiyo, jinsi watu walivyo na ndivyo hali yao itakavyokuwa.
   
 3. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sekta ya afya haitaweza kusonga mbele kama naibu wake ni mganga msaidizi, sipati picha alipewaje huo wadhifa. Na waziri ni daktari bingwa wa watoto (read misuse of a scarce human resource) kwa nini wasiwekwe watu waliosomea uongozi na mambo ya sera katika afya?
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hivi juzi kuna jamaa yangu ilibidi amtoe mgonjwa wake muhimbili baada ya kukutwa kalazwa chini ati "anangojea kitanda"..!
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Mar 24, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hii mbona iko tokea zamani....tokea niko shule ya msingi watu walikuwa wanalala chini hapo kwenye hospitali yetu kuu. Hakuna kipya, cha kushangaza, wala kushtua. Hali iko hivyo tokea zamani...

  Pengine haya mambo ya nationalized healthcare ndio madhara yake hayo.....
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wakuu... this is a very crucial topic, ila sijui hata nianzie wapi!

  KUna facets nyingi sana za kuiangalia muhimbili;

  • kwanza ni namna gani governance yake inakuwa affected na Tawala za mikoa na serikali za mitaa
  • we do also to position muhimbili role kwenye PPP
  • Nafasi nyingine kubwa kwenye hii discussion ni namna ya financing ya activities zake including equipment and fixtures zinavyotumika na kuwa accounted for
  • Isurance schemes zilizo pale
  • Role ya chuo (MUCHS)
  • Role ya research zinazoendelea
  • Role ya donor community
  • Role ya wizara mama na ofisi ya rais
  • Effort level ya staffs na remuniration
  • How it fits into the national health reform
  • How is muhimbili is planning to expand na any sustainable plans zake including franchise etc
  Nina imani kabisa, Muhimbili ikipata leaders wazuri, itaongoza mapambano ya kuinua afya. Na pia ikiumia PPP, management improvement and strategic positioning kuwa niche ya huduma mama

  otherwise tutaishia kuwa na hii below sub-standard health care delivery system nchini ambayo iko fragmented,l influenced by mediocrity hasa kutoka kwa staffs wa donor community na watanzania

  Natafakari namna ya kuanza kuingia kujadili health care system yetu hasa kwenye uongozi nakosa hata pa kuanzia kwani tumeweka madaktari kama viongozi wa management badala ya health administrations, health economists na business development and managers
   
 7. M

  Major JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2010
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Hata kama ungeweka management ya kiingereza kama serikali haiwezi kutoa fungu kwa ajili ya hii hospitali ni kazi bure,hata kama ungepewa wewe ambaye unasikia uchungu sana kama hakuna pesa ni kazi bure .yaani ni lawama tu
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  haya masuluhisho ndiyo ya fikra za kina Kikwete! tatizo likija wao suluhisho ni kumwaga fedha tu.. lingekuwa hilo ni suluhisho ATCL ingekuwa shirika bora, umeme nchini usingekuwa wa shida na elimu ingekuwa bora zaidi katika Afrika.. tatizo ni uongozi!
   
 9. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2010
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mwanakijiji hamna hata haja ya kufanya deep analysis kusolve hii healthcare debacle ya pale Tz especially Dar. Ni uongozi makini na kujali maisha ya wananchi tu ndicho kinachotakiwa.

  Serikali kwa kuanzia Dar, inaweza kabisa kuzifanya hospitali za Mwananyamala, Temeke na Ilala kuwa hospitali za mkoa na kuzijenga kwa hadhi hiyo kutokana na wingi wa wananchi wanaozizunguka.

  Ukishafanya hilo ndio mambo mengine ya kitaalamu yafuate, bila hilo tutabaki hivi hivi tunakufa kwa makosa ya kijinga na uzembe wa viongozi wetu na kuweka kipaumbele kwenye kununua VX na kujenga nyumba za kifahari za viongozi na kufanya semina kwenye mahoteli ya kifahari.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nasikia kujenga hospitali mpya ya wilaya ya Ilala kulikadiriwa kugharimu shilingi milioni 600! Kwa nyumba ya Gavana wenu tungeweza kujenga HOSPITALI MBILI!!
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Uongozi mbovu na kutojiamini kwa wasomi wetu ni tatizo kubwa sana.Kwa bahati mbaya hata wasomi wakubwa wanaoongoza taasisi kama hizi ambazo 100% zinaendeshwa kitaalamu nao wamesalimu amri kwa wanasiasa. Wanapelekeshwa kama matairi mabovu!!!
  Hakuna mwanasiasa anayeona umuhimu wa taasisi kama muhimbili leo maana wakiugua wanakimbilia India au nchi nyingine za nje kutibiwa. It takes courages and patriotic people at Muhimbili and other institutions to show that in some areas, things could be done differently without inolving politicians.
  Kwa bahati mbaya hawa wanataaluma hizi nyeti nao wanaona hawawezi kutoka bila kujiunga na wanasiasa. Tumefanya siasa kuwa na msururu mkubwa wa aspirants na ili kufanikiwa katika kujiunga nayo ni lazima kusalimu amri kwa wanaendesha siasa hizo hata kama gharama yake ni kuachilia mbali kifo cha professions zetu.
   
 12. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,713
  Likes Received: 3,119
  Trophy Points: 280
  Ubora wa Hospitali ya taifa Muhimbili utakuja iwapo hospitali za wilaya na mikoa zitaboreshwa kwanza in a way wagonjwa sio lazima waende Muhimbili kuna magonjwa mengine yanaweza kutibika hata kwenye hospitali za wilaya. Sasa wa kuboresha hizo hospitali za mikoa na wilaya ni nani? Ni serikali ambayo ina wabunge wake uchwara ambao kazi kupiga debe wakisahau ujenzi wa nchi ni kuanzia hapo ulipo sio mpaka uende Dar es Salaam uwaambie wananchi waliokupigia kura huko ndiko kuliko na suluhu. Wakuu wa Mikoa,Wilaya,serikali za mitaa, kata, na wabunge wote ni hopeless period.
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ni kweli kabisa, na hata kama serikali ingeweka pesa kiasi gani, kama hakuna mikakati sustainable na developmental hatufiki popote...

  Na ndio maana hizo point nilizoweka hapo zinategemeana na without proper planning hatufiki hata hao ABBOTT wakileta hadi gloves na dawa

  It is not that complicated though... waipige business plan inayoaddress stakeholders wote... amini nikuambiayo kwamba muhimbili haifaidiki ipasavyo na research, huduma za maabar na consultations kwani watu wajanja wameshaweka mirija

  Costing and financing are key in planning but management na leadership ni mhimili wake
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nashukuru mzee, baadhi tunadhani kila penye udhia ni kupenyeza rupia!!! kumbe kwingine si udhia bali ni "uzia"

  mabilioni ya kikwete, kweshnehi che, nk

  Turudi kuandika alif kwa kijiti
   
Loading...