JEMEDARI .H.
JF-Expert Member
- Oct 29, 2012
- 341
- 63
Hali ya usalama katika mji wa mtwara bado jeshi la polisi wakishilikiana na jeshi la wananchi j.w wanaendelea kufanya dolia ili kuzuia aina yeyote ya fujo inayoweza kujitokeza kutoka kwa wananchi wa mtwara ambao wanasubiri tamko la serikali kuhusu kuwepo au kutokuwepo mradi wa kutandika bomba la gas kwenda dar es salam kupitia wizara ya nishati na madini inayotegemewa kuwasirisha budget yake siku ya jumatatu.
Maeneo ya BIMA, Bank ya N.M.B. na CCM mkoa hali si kama kawaida kwani hakuna huduma za kijamii kama usafiri wa bajaji,taxi na boda pia maduka mahoteli yamefungwa kwa kuhofia vurugu hali ni hivyo hivyo katika maeneo ya soko kuu na stand kuu hakuna huduma ya kuuza vyakula,maduka na huduma ya mabasi kwenda mikoani.
Baadhi ya abiria waliojitokeza kupanda kwenye basi moja la kwenda vijijini walishushwa na kundi kubwa la vijana waliokusanyika stand hapo,pia ukionekana unapakia abiria kwenye boda au bajaji kundi hilo linazuia,licha ya magari ya FFU na JW kuendelea kuzunguka vijana wanaonekana kutokuyaogopa bali wanaendelea kusimama ktk makundi huku wakishangilia.
Lengo kuu la wanamtwara kusimamisha huduma za kijamii siku ya leo wanadai ni kufikisha ujumbe kwa serikali kuacha mala moja mpango wake wa kujenga bomba la gas asilia kupeleka gas Dar kwani wao wanataka mtwara iwe special energy zone,ambayo shughuli zote za production, procesing na exportation zifanyike kupitia bandari ya mtwara,na hata umeme utoke kwa njia ya nguzo kwenda Dsm
Naomba kuwasilisha moja kwa moja toka eneo la tukio
MADUKA YA BIMA YOTE CLOSED:
JUCTION YA BIMA HAINA WATU KABISA, HATA NMB IMEFUNGWA:
KWA MBALI UTALIONA GARI YA ASKARI IKIRANDARANDA...KOKOBICHI, KIMYA KABISA YANI
Tafuta kuna thread ya jana inahusu MTWARA KWANZA, GESI HAITOKI. Kwa ufupi, wakazi wamehamasishwa kusikiliza kauli ya serikali kuhusu geni iliyopatikana mikoa ya kusini leo kuanzia saa 3 wakati bajeti ya wizara husika itakapokuwa inasomwa bungeni.Ebu fafanua, kuna nini hasa?
Ebu fafanua, kuna nini hasa?
wananchi wapate fursa ya kutizama bunge, wafahamu hatma ya gesi ili hatua zichukuliwe "na wananchi wenyewe"
Tafuta kuna thread ya jana inahusu MTWARA KWANZA, GESI HAITOKI. Kwa ufupi, wakazi wamehamasishwa kusikiliza kauli ya serikali kuhusu geni iliyopatikana mikoa ya kusini leo kuanzia saa 3 wakati bajeti ya wizara husika itakapokuwa inasomwa bungeni.
Kweli Mungu anataka kuikomboa Tanzania dhidi ya Shetani .........................................wananchi wapate fursa ya kutizama Bunge, wafahamu hatma ya Gesi ili hatua zichukuliwe "na wananchi wenyewe"
Ngoja tusubiri updates kutoka kwa Wakuu Sizinga na THE BIG SHOW
Taarifa hizo ni za kweli,sizinga ataleta picha mda si mrefu sana
Ngoma inogile, aminia wamakonde. swali sasa hayo mabomuwaliyopeleka watayapiga wapi?[/QUOTE]
Ukizingatia hawajazoea kuona wananchi WAMETULIA (siyo kuandamana).........Itabidi mzigo wauweke AKIBA!!!!
Na hao watu wana nguvu sana na wanakubalika huko Mtwara. Ndio demokrasia huyo.mbona leo ni kuna muendelezo wa mjadala wa bajeti ya uchukuzi ya dr.mwakyembe..nani kawaambia leobajeti ya wizara ya nishati na madini...ukweli hili jambo la gas kuna watu wako nyuma ndio wanahamamsisisha wananchi vyema serikali ikawa makini na hawa watu wachache wanao chochea vurugu baada ya mshakamano na kuwaeleza wananchi ukweli.....