Hali ya mnyonge wa kweli wa nchi hii (Mkulima) 2015-2021 ikoje?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,220
12,724
Tumekuwa tunaaminishwa kuwa wanyonge wa nchi hii ni machinga, bodaboda, mamantilie, bajaji nk. Lakini hawa hawana unyonge wowote sema tu wanaplatform ya kuongea na kusikika. Ukipiga hesabu wengi wa hawa watu utakuta wako uchumi wa kati.

Mnyonge wa kweli wa hii nchi ni mkulima wa jembe la mkono huko kijijini. Huyu analia kimyakimya kwasababu hapewi/hana jukwaa la kuongelea. Mbayq zaidi hata wapinzani hawawajali watu hawa.

Laiti wapinzani wangejua nguvu ya wanyonge hawa na wangeuitumia leo wangekuwa na hali nyingine lakini wao nao wamekumbatia wanyonge feki (mama ntilie, bodaboda, bajaji, na machinga).

Sasa Rais wetu (RIP) alikuwa anajinasibu kuwa ni Rais wa wanyonge, naomba kujua hali ya wanyonge wa kweli (wakulima) toka 2015-2021 imekuwaje, imeboreka au imezidi kuwa mbaya?
 
Mnyonge ni yule anayenyongwa.
Mpaka sasa wakulima wengi matokeo i mbili bila. Mwendazake mbili na wakulima hatujapata kitu.
Gharama za kilimo haziendani na mauzo!
Siku hizi kisichoshambuliwa na wadudu ni nyasi tu.
Mazao yote tokea unapanda hadi unavuna, lazima dawa dawa!
Ukija kwenye masoko ndiyo hayaeleweki! Kifo cha utalii kimetuua wakulima wa nafaka, mbogamboga na matunda.

Raisi alikuwa raisi wa miundombinu na makusanyo na mapato na matumizi yaliyompendeza yeye.
Hakuwa raisi wa wakulima, aliua biashara ya mbaazi, akaja kwenye korosho, sijui wakenya aligombana nao kipi, mahindi nayo ikatibuka, mpaka anamaliza miaka 10, na hakika kusingekuwa na mfanyabiashara mkulima, Agribusiness ingekuwa historia.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Back
Top Bottom