Hali ya mafuta (NISHATI) ikoje huko uliko?

Robot la Matope

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
7,091
13,790
Hali mbaya imewakumba watu mbalimbali katika mikoa tofauti. Kama ilivyo ada, Jf we dare to talk openly, tupe hali halisi ya ulipo

tapatalk_1690813102620.jpg
FB_IMG_1690789330226.jpg
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano August 02, 2023 saa 6:01 usiku ambapo kwa mwezi Agosti 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ni Tsh. 3199 kwa lita, dizeli Tsh. 2935 na mafuta ya taa 2668.

Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Agosti 2023 yaliyoonesha kupanda kwa bei yanatokana na changamoto za upatikanaji wa Dola za Marekani, mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta.
#MillardAyoUPDATES
 
Jana Sikupata Nafasi Ya Kupiga Pictures Ila Moshi Mjini Kulikuwa Na Foleni Ndefu Sana
Majira Ya Saa Moja Kwenye Vituo Vya Total, Puma Vilivyopo Mjini
Wanasiasa Wapuuzi Sana Walituhakikishia Maneno Matupu Ghafla Bidhaa Haionekani
 
Back
Top Bottom