Hali ya kwenye media (TV) ni tete

njaakalihatari

JF-Expert Member
Feb 12, 2019
4,084
8,663
Nilikuwa jana na jamaa mmoja ambaye ni mtangazaji wa kituo kikubwa cha TV bongo ananimbia hali ya kifedha ya media nyingi haswa Tv ni tete,hapo sisemei magazeti ukiondoa yale ya michezo maana yana afadhali.

Anasema afadhali radio bado sponsors wako wengi haswa vipindi vya michezo na vile vyenye contents za uswahilini kama uhondo au leo tena.

Sababu kubwa ni mvuto wa tv kupungua kutokana na social media na kubanwa vitu vya kuandika na kusema haswa vya kisiasa,pia michezo haswa mpira wa miguu imekuwa na nguvu sana kwa hiyo vipindi vya michezo bado havikosi sponsors haswa vya redio maana gharama za kutangaza ni ndogo kuliko tv na wengi wanasikiliza.
 
Kwani siasa ndio habari pekee?

Wasivunge tu U tube kawameza habari kwisha.
 
Kuwa kwenye TV industry ni kama upo kwenye meli inayozama. Hapo mmoja avunje kituo chake atengeneze netflix ya kibongo
 
Waendelee tu na upuuzi wao wa kumtanfaxa huyo anayejiita mwendawazimu, namba ni lazima WAISOME TU! Mama.e

Nilikuwa jana na jamaa mmoja ambaye ni mtangazaji wa kituo kikubwa cha TV bongo ananimbia hali ya kifedha ya media nyingi haswa Tv ni tete,hapo sisemei magazeti ukiondoa yale ya michezo maana yana afadhali.

Anasema afadhali radio bado sponsors wako wengi haswa vipindi vya michezo na vile vyenye contents za uswahilini kama uhondo au leo tena.

Sababu kubwa ni mvuto wa tv kupungua kutokana na social media na kubanwa vitu vya kuandika na kusema haswa vya kisiasa,pia michezo haswa mpira wa miguu imekuwa na nguvu sana kwa hiyo vipindi vya michezo bado havikosi sponsors haswa vya redio maana gharama za kutangaza ni ndogo kuliko tv na wengi wanasikiliza.
 
Kwani siasa ndio habari pekee?

Wasivunge tu U tube kawameza habari kwisha.
Habari za siasa ndio maisha!!ndio maana kipindi ya jk, vyombo vya habari vilikuwa huru sana, mfano kipindi cha kipima joto/malumbano ya hoja kwenye kituo cha ITV, ukienda chaneli ten, unakutana na generali on monday wadhamini lazima tu wajitokeze kwani ni watazamaji wengi wanatazama!!na hats taarifa za habari zilikuwa zinaonyesha maonevu ya serikali dhiti ya wananchi, lakini sasa utaona malalamiko ya wananchi dhiti ya mwekezaji na sio serikali!!yaani kwa sasa huwezi tofautisha taarifa ya habari ya ITV, na ile ya TBC!!!Hapo utegemee nini?na vitafungwa kabisa
 
Maendeleo ya Teknolojia hayazuiliki

Tanzania tunapitia kwenye haya mabadiliko ya Teknolojia plus mabadiliko ya uchumi na siasa. Na kwa maana hiyo jamii inahitaji zaidi vitu vitakavyoweza kuwasaidia. Mimi binafsi nyumbani kwangu sijui hata Tv inavyowashwa, Mimi sio mteja wa program ZA t.v. sababu hakuna ninachopata humo zaidi ya taarifa ya habari

Sasa ndio muda muafaka kwa wenye t.v., radio na magazeti kukaa chini na kufanya tathmini yatakayoweza kupelekea mageuzi ya programs zao yaendane na uhitaji wa sisi walaji

Kwenye haya mabadiliko wenye medias washirikiane na wadau wengine wenye mawazo chanya wanapata mengi
 
Pamoja na mitandao kuikimbiza industry ya media hasa tv bado baadhi yetu hatujui kama media zimebamwa na mfumo wa kisiasa.

Mfano kwa sasa huwezi kwenda kufanya investigation story na kumhoji kiongozi wa serikali au wananchi pasi ruhusa.

From that point utaona maji yapo shingoni na tasnia imebaki kuwa ya 'kitambulisho cha mwandishi' kuandika habari nyepesi zisizohumiza.
 
Maendeleo ya Teknolojia hayazuiliki

Tanzania tunapitia kwenye haya mabadiliko ya Teknolojia plus mabadiliko ya uchumi na siasa. Na kwa maana hiyo jamii inahitaji zaidi vitu vitakavyoweza kuwasaidia. Mimi binafsi nyumbani kwangu sijui hata Tv inavyowashwa, Mimi sio mteja wa program ZA t.v. sababu hakuna ninachopata humo zaidi ya taarifa ya habari

Sasa ndio muda muafaka kwa wenye t.v., radio na magazeti kukaa chini na kufanya tathmini yatakayoweza kupelekea mageuzi ya programs zao yaendane na uhitaji wa sisi walaji

Kwenye haya mabadiliko wenye medias washirikiane na wadau wengine wenye mawazo chanya wanapata mengi
Wakiwafurahisha watazamaji wataikosea serikali,serikali inataka tu kusifiwa,wananchi wanataka kero zao zisemwe kwa uwazi,kwa hiyo hapo ku a upanga ukatao kuwili,amua kuwa upande wa wateja au upande wa serikali,ila kote kote ni hatari kwako mwekezaji,mi bado naangalia ITV!! Japo kwa shingo upande
 
1098090.jpg
 
Wananchi zaidi ya 84% wanaipenda na kuielewa serikali yao, na wanatamani kupata vitu vinavyowajenga kama mipango ya serikali inavyoelekeza
Kwa hiyo ondoa shaka, hapawezi kuwa ugomvi wa taabu kwa serikali wala umma wa watanzania
 
Back
Top Bottom