Hali ya kupooza kwa mwanadada Wakonta

Kupitia binti Wankota nimemuona Mungu kwa namna ya ajabu sana, nimeona Mali, uzuri, elimu, vya dunia hii, vinaweza zimika dakika yoyote,,hakuna binadam mwenye mamlaka navyo.
Hata mimi nimeguswa sana na huyu dada, sisi tuliowazima tushukuru sana mungu, hebu fikiria unasaidiwa kuanzia kupiga mswaki, kunawa uso, kula, hata kulala mpaka kuamka, mungu awatie nguvu wanaomhudumia maana wanamtihani mkubwa, fikiria ukijisaidia hajui kama kajisaidia mpaka umuangalie, mungu naomba tuepushe na mitihani mikubwa kama hii........nakijaliwa kupata mtoto wa kike nitampa jina la WAKONTA
 

Na bado Wakonta amevaa sura ya furaha, sioni chuki akiongea.
 
Mkuu hiyo ahadi usipo itimiza litakalokupata shauri yako mwenyewe
Cc mshana jr
 
Kama hospitali haiwezekani basi apelekwe kwenye huduma ya kiroho kwa TB Joshua kwa maana wiki iliyopita niliona mtu aliyepooza kule Korea akisimama toka alipokuwa amelala. Inawezekana shetani kaweka mkono wake
 
Mmh binadamu tunavyojuaga kulalamika. Mtu ana ndoto ya kufanya kitu fulani, basi isipotimia, atakavyolalamika kwa Mungu asahau na mema mengine yote mweee

Nahisi ujasiri wa huyu binti umetibu tabia za watu wengi kwa sasa, nahisi kila Mtu amejikosoa na kumshukuru Mungu.
 
Pole sana Wakonta popote pale ulipo Mwenyezi akulinde kwa hali uliyonayo.
 
Kuna mpanda farasi fulani nimesahau jina...naye alivunjikaga shingo, akabaki na kontroli ya kichwa sijui kama yuko hai. Dada Mungu atamsimamia..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…